Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mwinyi aipa Tira kongole kupunguza matumizi nje ya nchi

Muktasari:

  • Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi, ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (Tira) kuanzisha mpango wa kupunguza kiwango kikubwa cha fedha zinazotumika nje ya nchi badala yake kutumika ndani.

Unguja. Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi, ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (Tira) kuanzisha mpango wa kupunguza kiwango kikubwa cha fedha zinazotumika nje ya nchi badala yake kutumika ndani.

Dk Mwinyi ameyasema hayo leo Septemba 4, 2023 Ikulu ya Zanzibar alimpozungumza na uongozi wa mamkala hiyo uliofika kwa lengo la kuwatambulisha mabalozi wapya wa kuitangaza taasisi hiyo kwenye ngazi ya viongozi wakuu wa Serikali za SMZ na SMT, Mashirika ya Umma na taasisi nyingine.

Dk Mwinyi amesema kwa miaka mingi Serikali ilikuwa ikikata bima nje ya nchi sasa Tira imeleta mafaniko makubwa kwa kuokoa fedha nyingi.

“Zilikuwa zinakatiwa bima nje ya nchi lakini kwa sasa bima zinakatwa ndani na kuokoa kiwango kikubwa cha fedha,” amesema

Dk Mwinyi amewapongeza mabalozi wapya walioteuliwa na Tira kuendelea kuitangaza taasisi hiyo kwa viongozi wa umma wa Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Viongozi hao ni Katibu Mkuu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Zena Ahmeid Saidi, Wanu Hafidh Ameir na Japhet Hasunga wote ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naye, Kamishna wa Bima Dk Baghayo Saqware amesema kuna mafanikio yamepatikana kwenye sekta ya bima ikiwa ni pamoja an ongezeko la asilimia 1.68 kwenye pato la Taifa kwa mwaka 2021 kutoka asilimia 0.56 kwa mwaka 2020.

Pia amesema taasisi hiyo imeendelea kuongeza gawio kwa Serikali kutoka Julai 2022 hadi Juni 2023 kwa kulipa gawio la Sh2.9 bilioni.

Akizungumzia mafanikio kwenye sekta ya ajira, Kamishna Saqware amesema hadi kufikia septemba mwaka 2022 Tira, imetoa ajira z kudumu kwa Watanzania 4, 173 ikilinganishwa na ajira 3,208 kipindi kama hicho mwaka 2021.

Mabalozi hao wa Tira, waliteuliwa Februari mwaka huu, wakikabidhiwa majukumu ya kutoa ushauri kwa Mamlaka na sekta ya bima kwa ujumla kuhusu maendeleo ya sekta hiyo pia kutoa elimu kwa umma juu ya masuala ya bima katika ngazi mbalimbali ikiwemo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi.