Dk Ndugulile ateuliwa IPU kushauri masuala ya afya

Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile.

Muktasari:

  • Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) umemteua aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya Tanzania, Dk Faustine Ndugulile kuwa mjumbe wa Kamati ya kushauri masuala ya afya wa Umoja huo.

Dar es Salaam. Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile ameteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya ushauri masuala ya afya ya Umoja wa Mabunge duniani (Inter-Parliamentary Union).

 Uteuzi huo unaofanywa na Rais wa umoja huo wa mabunge duniani Duarte Pacheco, unamfanya Dk Ndugulile kuwa sehemu ya wabunge 12 duniani wanaoishauri IPU kuhusu masuala mbali mbali yanayohusu afya.

Dk Ndugulile ambaye amewahi kuwa Naibu Waziri wa Afya na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, uteuzi wake uliofanyika Februari, 2023 utadumu kwa kipindi cha miaka minne.

Dk Ndugulile ni daktari mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 25 kwenye afya ya jamii ndani na nje ya nchi.

Pia ameshawahi kuwa mwakilishi wa bara la Afrika katika Taasisi ya kimataifa ya Ukimwi na mwanzilishi wa mtandao wa dunia kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu (TB).