Kauli ya kwanza Dk Ndugulile baada ya kutenguliwa

Kauli ya Dk Ndugulile baada ya kutumbuliwa

Muktasari:

  • Aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumpa fursa ya kuwa waziri.

  

Dar es Salaam. Aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumpa fursa ya kuwa waziri.

Juzi Samia alifanya mabadiliko madogo katika baraza la mawaziri kwa kutengua uteuzi wa mawaziri watatu akiwamo Ndugulile na kuteua wapya wanne ambao ni Dk Ashatu Kijaji,  Dk Stergomena Tax,  January Makamba na Profesa Makame Mbarawa.

Ndugulile uteuzi wake ulienguliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Dk Kijaji ambaye ni mbunge wa Kondoa Vijijini.

Ndugulile ameandika hayo jana Jumatatu Septemba 13, 2021 kupitia mtandao wa kijamii amewashukuru wadau wa Tehama kwa ushirikiano waliompa na ametoa pongezi kwa Kijaji kuteuliwa.


“Namshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kunipa fursa ya kuhudumu katika Serikali yake. Nawashukuru Wizara na taasisi zake kwa ushirikiano walionipa. Nashukuru wadau wa Tehama kwa ushirikiano mlionipa. Hongera sana Dk Ashatu kwa kuteuliwa. Kazi Iendelee” ameandika.