Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Osati ahoji sababu ya bima ya afya kwa wote kucheleweshwa

Daktari Elisha Osati

Muktasari:

  • Kucheleweshwa kwa mpango wa bima ya afya kwa wote kumetajwa kuwa chanzo cha malalamiko ya mabadiliko ya mfumo wa Toto Afya kadi ulioanzishwa na NHIF

Dar es Salaam. Daktari Elisha Osati amehoji sababu ya Serikali kuchelewesha mfumo wa Bima ya Afya kwa wote. 

Ameyasema hayo leo Septemba 20 wakati wa mjadala wa X-Space iliyoandaliwa na Mwananchi Communications Ltd wenye mada ya ‘Mabadiliko ya huduma ya Toto Afya kadi nini sababu na suluhisho lake.’

"Bajeti ya Wizara ilipita haikuzungumzia kitu chochote, nafikiri NHIF (Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya) inajua sababu za ndani kwa sababu Serikali ilitakwa kuweka hela ili huduma iweze kuanza," amesema.

Amesema wakati NHIF ikihamishia suala la Toto Afya kadi watoto shuleni, hakuna juhudi za mfuko huo kutoa elimu kwa wazazi. 

"Hatujaona NHIF ikizungumza na Tamisemi (Ofisi ya Rais) na idara zingine kuhamasisha wazazi watoto wajiunge na mfuko. 

"Mimi ni mmwenyekiti wa moja ya bodi ya shule sijawahi kuwaona NHIF wakija kusisitiza watu kujiunga na bima kwa gharama zinazotakiwa," ameeema Osati amesema.

Pia Ostai amesema kuna mifuko mingi ukiwemo Mfuko wa Afya ya Jamii (CHIF) iliyoboreshwa ambayo ilikuwa inatumika chini, lakini ulionekana kulketa mfutano kati ya NHIF na CHIF.

Amesema wenye mamlaka hawajatoa majibu sahihi kuhakikisha bima inapatikana kwa watu hakuna mipango ya makusudi ya kuunganisha mifuko miwili ili watu kupata matibabu, haya mambo yanahitaji maamuzi ya makusudi.

Kwa upande wake Tumaini Makole Mtaalamu wa Famasia amesema watu wengi hawana elimu ya bima kwahiyo NHIF waongeze nguvu ili kuwafikia wananchi na kuwapatia bima.

"NHIF watoke ofisini na kuwafuata wananchi kuwahamasisha wananchi kujiunga na bima, kwahiyo tunataka wananchi wakafuatwe mitaani," amesema Makole.

Pia Makole amesema kuwe na usimamizi mzuri wa mfuko uimarishwe kile kilichopo kwenye mfuko kitumike vizuri, magonjwa yanayowasumbua watoto yanazuilika.

Pia amependekeza kuwe na mpango wa muda mrefu wa kugharamia matibabu kwa kuchangia kidogo kidogo.

Hata hivyo, akijibu hoja hizo, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga amesema huwa hawaendi kutoa elimu kwa watoto bali kwa wazazi wao. 
“Mijadala ya Toto Afya Card bado inaendelea na kuna shule zimesema zitajiunga mapema Januari mwakani. Bima ya afya kwa wote ni mchakato ambao unaendelea kwa sasa hatujakwamia njiani na tupo makini kama nchi, tunataka tukianza tumeanza ili tuwe mfano kwa mataifa mengine,” amesema.