Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dudu Baya anashikiliwa Oysterbay

Godfrey Tumaini maarufu  ‘Dudu Baya’ 

Muktasari:

Amefunguliwa makosa ya matumizi mabaya ya mtandao

Mwanamuziki Godfrey Tumaini maarufu  ‘Dudu Baya' anashikiliwa na polisi katika kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa polisi Kinondoni, Mussa Taibu amesema Msanii huyo anashikiliwa kwa mahojiano.

Dudu Baya aliyewahi kutamba na wimbo Mwanangu Huna Nidhamu, alikamatwa jana Februari 27, 2019 baada ya kuamriwa na Baraza la Sanaa la Taifa kufanya hivyo.

Jana, Waziri wa Habari na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe aliagiza Jeshi la Polisi na Basata wamchukulia hatua mwanamuziki huyo kwa makosa ya kumkashifu, aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji, Ruge Mutahaba.

Baada ya amri hiyo, Basata ilimtaka mwanamuziki huyo kujisalimisha katika kituo cha polisi Oysterbay asubuhi ya leo.

Mwanamuziki huyo ameshtakiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya mtandao.