Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Figisu mradi wa maji watua kwa RC

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu akizungumza na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha.

Muktasari:

  • Hujuma mradi wa maji wa Gararagua uliotumia zaidi ya Sh1.7 bilioni na kugawa watendaji na madiwani umemwibua Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, kutafuta suluhu ya haraka na ya kudumu.

Siha. Malalamiko ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha kuhusu hujuma katika mradi mpya wa maji wa Gararagua, ulioigharimu Serikali zaidi ya Sh1.7 bilioni, yametua kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu.

Kutokana na malalamiko hayo, RC huyo ameamua kutafuta suluhu ya haraka ya mgogoro huo unaoonekana kuanza kuwagawa watendaji wa Serikali pamoja na madiwani, akilenga kuyawahi maamuzi ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso yanayokusudiwa kutolewa wiki ijayo.

Uamuzi wa Babu kushughulikia malalamiko hayo, umetokana na tishio la madiwani wa halmashauri hiyo kutaka kufanya maandamano ya amani kupinga hujuma dhidi ya mradi huo, unaohusishwa na matumizi ya fedha za umma.

Jana, akiwa wilayani Siha, ambako aliitwa kusikiliza malalamiko hayo, RC Babu alisema: "Yote haya ambayo mnazungumza madiwani kwa uchungu sio kwamba mnataka kumwonea mtu, ninyi ni wawakilishi wa wananchi katika maeneo yenu.”

"Nataka niwathibitishie na kuwahakikishia kuwa katika kipindi hiki ambacho Waziri wa Maji, Jumaa Aweso hajafika hapa, nitakwenda kufanya kazi usiku na mchana kuanzia kesho. Naleta timu hapa kutoka Ruwasa mkoani, waje wasaidiane na mhandisi wa maji hapa wilani ili kujua chanzo cha tatizo,” amesema.

Novemba 8, mwaka huu baraza la madiwani la wilaya hiyo, lilijikuta wajumbe wake wakigawanyika kutokana na malalamiko hayo lakini waliungana baadaye na kuazimia kuandamana ili kuishinikiza Serikali ngazi ya mkoa kuingilia kati.

Hoja hiyo iliibuliwa na Diwani wa Kata ya Endumenti, Vicenti Kileo ambaye alisema mara kadhaa wamekuwa wakihoji kuhusu mradi huo na hawapewi majibu yenye kuridhisha.

"Hili tatizo halijachukuliwa kwa umakini wake, Mwenyekiti naomba mturuhusu kila kata itoe waandamanaji 2000 tuje hapa ili meseji hii ifike juu (kwa Rais), kama unaenda ngazi inayostahili kuuliza na hupati msaada maana yake uende ngazi ya juu uonekane," alisema na kuongeza;

"Nasema kwa machungu kwa sababu mimi niko kwenye chanzo cha maji lakini hakuna maji, ukiuliza unapewa majibu ya rejareja. Tunaona njia rahisi ambayo inaweza kutusaidia tupaze sauti ili hawa wamama na watoto angalau waweze kupata nafuu kidogo ya maji, tutengeneze maandamano ya amani pengine tutasaidiwa kwa wakati."

Naye diwani wa Kata ya Sanya juu, Juma Jani amesema kwa kile kinachoendelea katika mradi huo wa maji wanadanganywa na hakuna majibu yanayoeleweka.

“...naomba mnielewe, mimi sio muumini wa kurumbana na wataalam, na wala sio muumini wa kupenda maandamano. Lakini nimesema sisi binadamu tukishindwa hata mawe yatasema...kwenye jambo hili natoa muda, nina waapia...tukitoka kata nzima... ujumbe utafika kwa Rais," amesema Jani.

Mgogoro ulianzia hapa

Jonathan Nassari, Diwani Kata ya Orkolili amesema: "Huu mradi tunaouzungumzia hapa baraza la madiwani tuliukataa, usipokelewe kwa sababu matatizo yalikuwa yanaonekana. Huu ni mwezi wa pili sasa hakuna maji katika maeneo ya Mkombozi, na Orkolili hakuna maji, mara unaambiwa ni tope limeziba yaani hawaeleweki.”

"Leo tunajibiwa kisisasa hakuna maandishi yanayoonyesha kitu kinachofanyika hapa, haya maandamano ya jumla tutakayofanya ni kidogo sana, wala hatusemi polepole na hatuwezi kuishi bila maji alafu kuna watu wanakuja hapa wanakula fedha.

Tanataka mkandarasi aje hapa aondoe bomba zote aweke bomba mpya ili tuweze kutulia, tukiendelea kukosa maji mwezi wa tatu alafu ndio tutaelewana vizuri, hatutaweza kuvumilia kwa hali inavyokwenda, wala hatutaelezana kwa woga, tunachotaka ni maji na Serikali ipo."

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Dancan Urassa, alijaribu kuzima maandamano hayo akiwataka madiwani hao kutoyafanya na kwamba wawe na subira wakati jambo hilo likitafutiwa ufumbuzi wa kudumu.

"Kama ni maandamano naomba msihamsishe maana hata mimi nimezuia maandamano, niwaombe mtulize 'presha' tumpe nafasi Mkuu wa Mkoa kufahamu tatizo la mradi kwa sababu lazima aje," alionya Urassa

Ili kufifisha uamuzi huo wa madiwani, Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) Wilaya ya Siha, Kondo Said, alisema wanachokifanya kwa sasa ni kubadilisha mabomba yaliyowekwa kwa kipimo cha kipenyo cha inchi sita na kuweka mengine mapya.

"Huu mradi wa Gararagua, bomba zilizopo pale ni za inchi sita ambazo zilikuwa zinapasuka kila mara, lakini mradi huo kwa sasa unatekelezwa na wanabadilisha zile bomba za inchi sita wanaweka za inchi nane," amesema Said