Flaviana Matata agawa vifaa vya shule Msata

Mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata akiwa amembeba mmoja wa wanafunzi wa shule ya Msata kidogo kabla hajawakabidhi vifaa

Muktasari:

Flaviana aligawa vifaa hivyo  kwa wanafunzi   wapatao  345   akisindikizwa  na Mbunge  wa Chalinze  Mheshimiwa  Ridhiwani  Kikwete.

Na Mwandishi  Wetu,

Chalinze. Mwanamitindo wa Kimataifa Flaviana Matata  imetoa vifaa vya masomo kwa  wanafunzi wa Shule ya Msingi  Msinune iliyopo  Msata  Katika Wilaya ya Chalinze  Mkoa wa Pwani.

Flaviana aligawa vifaa hivyo  kwa wanafunzi   wapatao  345   akisindikizwa  na Mbunge  wa Chalinze  Mheshimiwa  Ridhiwani  Kikwete.

Akizungumza  kabla ya kukabidhi  vifaa hivyo Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Matata Foundation alisema kuwa  , taasisi hiyo ilianza  kufanya  ukaarabati katika Shule hiyo mwaka 2016 huku akisema kwamba akilinganisha hali ilivyokua  awali na sasa ni tofauti kwani  majengo yalikua chakavu tofauti na sasa ambapo wameweza kufanya ukarabati  , kuweka miundombinu ya  maji na umeme. Aidha  Matata aliongeza  kwa kusema kuwa  taasisi hiyo baada ya kumaliza  kukarabati majengo  hali  ambayo imeweka mazingira  rafiki  kwa wanafunzi, hivi sasa wanajipanga kujenga nyumba   za waalimu  huku akimuomba Mbunge wa Chalinze kusaidia baadhi ya vifaa vya  ujenzi ili kwa pamoja waweze kulifanikisha lengo hilo.

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na wanafunzi pamaoja na wazazi katika shule ya Msata

Akizungumza  kwenye mkutano huo mbunge wa  Jimbo la Chalinze Ridhiwani  Kikwete alisema kuwa amepokea kwa mikono miwili ombi la  ujenzi wa  nyymba za Waalimu kwani  katika taasisi zetu  bado tunachangamoto   nyingi lakini kwa  kupitia Taasisi ya Flaviana Matata Foundation nina imani wote  kwa pamoja tutaunganisha nguvu kwa kutumia mfuko  wa Jimbo nyumba hizo za Waalimu tutazijenga.

"Flaviana umetupiga  teke  kutoka mbali kwani ukirudi miaka 20 nyuma wakazi wa Kijiji hiki cha Msinune hawakuwa na mwamko wa elimu tofauti na ilivyo sasa nakiri hilo" alisema  Kikwete huyo.

Alisema kuwa ana anamuomba Mwanamitimdo huyo wa Kimataifa kuwatatulia changamoto ya soko la  zao la Mananasi ambapo kwa kupitia Taasisi yako  unayo nafasi ya  ya kutusaidia  karika  kututafutia fursa  za soko la mananasi nje ya nchi  ikiwa ni katika kukuza uchumi wa Chalinze.

Kila inapofika mwanzo wa Muhula Taasisi ya Flaviana Matata hupeleka vifaa vya shuleni ,pia kwa kupitia Taasisi hiyo  wamekuwa  wakitoa udhamini kwa wanafunzi katika   Shule za Sekondari na Vyuo Vikuu nchini.

Wakati huohuo Flaviana Matata ametoa wito kwa wazazi kuacha kuwakatisha   watoto wao wa kike masomo na kukimbilia kuwacheza ngoma.

"Baba zangu na  mama zangu nawaomba sana  muachane na tabia ya kuwakatisha masomo  mabinti zenu kwani elimu ndiyo ufunguo  wa maisha  hivyo wakati  umefika sasa wa kuachana na  mila potofu ambazo zinapoteza matumaini ya njozi zao katika  maisha  yao  ya baadaye wao wakiweza  kusoma watakuja kuwa msaada mkubwa sana kwenu na kwa jamii nzima kwa ujumla.”