Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gharama za uwekezaji zahamasisha vijana kuwekeza nchini

Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kampuni ya uwekezaji ya Joasamwe, Kapocha Masatu akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampuni hiy ya "Cello tapes" iliyopo Nyakato Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza. Picha na Anania Kajuni

Muktasari:

Kupunguzwa gharama za uwekezaji kwa wazawa kutoka Dola za Kimarekani 100,000 hadi 50,000 pamoja na msamaha wa kodi kumetajwa kuongeza chachu kwa vijana kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini. 

Mwanza. Kupunguzwa gharama za uwekezaji kwa wazawa kutoka Dola za Kimarekani 100,000 hadi 50,000 pamoja na msamaha wa kodi kumetajwa kuongeza chachu kwa vijana kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa wa kampuni ya uwekezaji ya Joasamwe, Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni hiyo iliyopo Nyakato Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Kapocha Masatu ameipongeza Serikali akidai punguzo hilo limehamasisha vijana na watanzania kuwekeza nchini.

“Niipongeze sana Serikali kwa kupunguza gharama za uwekezaji kwa wazawa kitendo ambacho kinatoa hamasa kwa sisi wazawa kuwekeza katika maeneo tofauti,”amesema Masatu 

Katika uzinduzi wa kampuni hiyo inayozalisha ‘cello tapes’ ulioambatana na chakula chakula cha pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu, Masatu ametaja changamoto zinazokwamisha utendaji kazi kuwa ni ukosefu wa umeme wa uhakika wa kuendeshea mitambo unaosababishwa na kukatika katika, uhaba wa malighafi ambazo wanaagiza nje ya nchi na ukosefu wa vyombo vya kusafilishia bidhaa hizo. 

Meneja wa Sido Mkoa wa Mwanza, Bakari Songwe ametoa wito kwa vijana wazawa kuiga mfano wa mwanzilishi na mkurugenzi wa kiwanda hicho ambaye ni zao la Sido kutafuta maarifa ili kujikomboa katika lindi la ukosefu wa ajira na umaskini. 

“Nitoe wito kwa vijana wa Kitanzania kuwa fursa zipo ni wenyewe tu kufanya bidii ya kuzitafuta ili wazitumie sisi Sido tupo hapa kwa ajili ya kutoa huduma hiyo nawakaribisha kuja katika ofisi zetu na kupata elimu na ufafanuzi wa namna ya kuanza na kuwekeza,”amesema Songwe 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho, Katibu Tawala Manispaa ya Ilemela, Marium Msengi mbali na kutoa pongezi kwa uongozi wa kiwanda hicho pia ametoa wito kuzidi kushirikiana na Serikali na wananchi ikiwa ni pamoja na kushiriki katika kuboresha huduma za jamii. 

“Wananchi nyie ni mashahidi Joasamwe kimeendelea kuunga jamii mfano walishiriki katika ujenzi wa zahanati hivyo nitoe rai kwao kwamba wasichoke wazidi kutuunga mkono katika shughuli mbalimbali kwa sababu bado tunaendelea kuleta maendeleo kwa wananchi wetu na nguvu ya wadau inahitajika,”amesema Msengi