Gwajima afika bungeni kuhojiwa

Gwajima aifika bungeni kuhojiwa

Muktasari:

  • Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima amefika kuhojiwa katika Kamati ya Bunge haki, maadili na madaraka ya Bunge leo mchana akiwa amevalia suti nyeupe yenye mshazari ya blue.

Dodoma. Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima amefika kuhojiwa katika Kamati ya Bunge Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge leo mchana Jumatatu Agosti 232, 2021.

Askofu Gwajima amefika saa 6.36 mchana akiwa katika gari nyeusi. Alipofika katika geti kubwa linalotumiwa na wabunge kuingia bungeni alipokelewa na askari wawili mmoja akiwa amevalia nguo za polisi na mwingine nguo za kiraia.

Mashine ilivyomgomea Askofu Gwajima akiwasili kwenye kamati ya maadili

Askofu Gwajima akiwa ameongoza na askari hao alielekezwa kukaa katika viti vilivyoko baada ya mashine ya kukagua iliyoko katika jengo la utawala akisubiri kuitwa ukumbini.
Endelea kufuatilia Mwananchi