Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hali ilivyo Kituo cha Polisi Lulembela kilichovamiwa na wananchi

Kituo cha Polisi Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita

Muktasari:

  • Wafanyabiashara wamepata hofu kufungua maduka kutokana na vurugu zilizoibuka jana baina ya wananchi na polisi na kusababisha watu wawili kufariki dunia.

Picha za hali ya kituo cha Polisi Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita baada ya jana Jumatano Septemba 11, 2024 kuvamiwa na wananchi huku wakifanya uharibifu wa baadhi ya mali ikiwamo gari.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime katika taarifa yake jana Jumatano kuhusu tukio hilo, alisema chanzo cha vurugu hizo ni baada ya watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba watoto wawili na wananchi waliokuwa kwenye mnada wa Lulembelea kuwadhania ni wezi wa watoto kisha  kuwashambulia.

“Walipokuwa wanawashambulia alitokea ofisa mtendaji wa kata  akawabeba kwenye pikipiki na kuwapeleka katika Kituo cha Polisi Lulembela baada ya watu hao kwenye gari, akawapeleka kituoni, hata hivyo wananchi takribani 800 walifika kituoni na kuwataka polisi wawakabidhi watuhumiwa hao ili wawaue," amedai Misime.

Amesema licha ya askari polisi kuwaelimisha na kuwaeleza ni kosa kujichukulia sheria mkononi, wananchi hao walikaidi na kuanza kukishambulia kituo cha polisi kwa mawe wakilazimisha kuwachukua watu hao wawili kwa nguvu ili wawaue.

Gari lililochomwa moto na wananchi nje ya Kituo cha Polisi Lulembela  


Gari lililochomwa moto na wananchi nje ya Kituo cha Polisi Lulembela  


Baadhi ya maduka yakiwa yamefungwa katika eneo Lulembela  


Baadhi ya maduka yakiwa yamefungwa katika eneo Lulembela