Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hitilafu yakwamisha treni ya SGR Dar-Dodoma

Muktasari:

  • Hitilafu hiyo iliyotokea imesababisha kuvurugika kwa ratiba za treni za kisasa (SGR) jambo ambalo limesababisha usumbufu kwa wasafiri

Dar es Salaam. Hitilafu iliyotokea katika mifumo ya uendeshaji wa treni ya kisasa ya umeme (SGR)   imesababisha mvurugiko wa ratiba za treni hiyo jambo ambalo limewafanya baadhi ya abiria kukwama katika stesheni tofauti.

 Abiria hao waliokuwa wakisafiri kwa nyakati tofauti leo Jumapili Novemba 3, 2024 walijikuta njia panda baada ya muda ambao walipaswa kusafiri kufika lakini safari hazikufanyika bila taarifa yoyote kutolewa.

Kutokana na hali hiyo, Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa taarifa kwa umma kwa kuwaomba radhi abiria na watumiaji wa usafiri huo huku ikiweka bayana mafundi wapo eneo la tukio wakifanyia kazi changamoto hiyo.

“Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaomba radhi kwa abiria wa treni ya mchongoko (emu) walioanza safari yao Dar es Salaam kwenda Dodoma saa 2:00 asubuhi na kusimama ghafla saa 2:20 kati ya Pugu na Soga. Pia tunaomba radhi pia kwa abiria wetu wa treni ya saa 11:15 alfajiri kutoka Dodoma na treni ya saa 3:30 kutoka Dar es Salaam ikijumuisha safari nyingine za siku ya leo ambazo zimeathiriwa,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

 Treni ya mchongoko inakwama ikiwa ni siku ya tatu tangu ianze kufanya kazi ya usafirishaji abiria kati ya Dar es Salaam na Dodoma. Novemba Mosi, 2024 ndiyo ilianza rasmi kazi ikitokea Stesheni ya Magufuli mkoani Dar es Salaam hadi Stesheni Kuu ya Samia mkoani Dodoma.

Treni hiyo ina vichwa mbele na nyuma tofauti na treni zenye kichwa kimoja, huku ikibeba jumla ya abiria 589 na inatembea kwa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa.


Endelea kufuatilia mwananchi kwa taarifa zaidi