Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hukumu kesi ya Ditto dhidi ya DSTV yaahirishwa

Mwanamuziki, Lameck Ditto (mwenye kofia) akiingia kwenye chumba (court) cha Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam sanjari na mawakili wake, Elizabeth John na Ally Hamza na meneja wake, Rodney Rugambo (mwenye fulana nyeupe). Picha na Imani Makongoro

Muktasari:

  • Ditto alifungua kesi ya madai mwaka 2020, akiiomba Mahakama iamuru Kampuni ya Multichoice Tanzania imlipe fidia ya Sh6 bilioni kwa kutumia wimbo wa Nchi Yangu aliodai ni wake, kwenye matangazo yao ya biashara bila ridhaa yake wakati wa kampeni za fainali ya Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2019

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeahirisha hukumu ya kesi ya madai ya mwanamuziki Lameck Ditto dhidi ya Kampuni ya Multchoice Tanzania Limited, maarufu DSTV iliyokuwa itolewe leo Jumanne Julai 16.

Hukumu hiyo sasa itatolewa Julai 22, 2024 mahakamani hapo mbele ya jaji mfawidhi, Salma Maghimbi.

Wakili wa Ditto, Elizabeth Mlemeta ameiambia Mwananchi Digital kwamba hukumu hiyo sasa itatolewa Julai 22.

Ditto ambaye jina lake halisi ni Dotto Bwakeya alifungua kesi ya madai mahakamani hapo mwaka 2020 akiiomba iamuru kampuni Multichoice Tanzania imlipe fidia ya Sh6 bilioni kwa kutumia wimbo  wa Nchi Yangu aliodai ni wake kwenye matangazo yao ya biashara bila ridhaa yake wakati wa kampeni za  fainali ya Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2019.

Pia, ameiomba Mahakama iamuru alipwe Sh200 milioni kutokana na madhara ya jumla, pia alipwe riba ya asilimia 25 tangu siku alipofungua shauri hilo akidai kampuni hiyo imemnyima fursa ya kunufaika na kazi yake.

Katika kesi hiyo, Ditto alipeleka mashahidi watano na DSTV ilikuwa na mashahidi wawili, Astrid Mapunda na Johnson Mshana wakiongozwa na mawakili, Simon Lyimo na Thomas Mathias.

Upande wa Ditto, baadhi ya mashahidi wake walikuwa ni produzya wa wimbo huo, Emmanuel Maungu (Emma the boy), meneja wa Ditto, Rodney Rugambo na Angela Karashani wakiongozwa na mawikili, Ally Hamza na Elizabeth Mlemeta.