Ijue aina ya ndege ya ATR 42-500 iliyopata ajali Bukoba

What you need to know:

Ni uzao wa tatu wa ndege za familia ya ATR 42 zinazotengenezwa na kampuni ya ATR, ambayo ni ushirika Aerospataiale ambayo inaitwa sasa inaitwa Airbus na Aeritalia ambayo sasa inaitwa Leonardo SPA.

China. Ndege ya ATR 42-500 ni uzao wa tatu wa ndege za familia ya ATR 42 zinazotengenezwa na kampuni ya ATR, ambayo ni ushirika Aerospataiale ambayo inaitwa sasa inaitwa Airbus na Aeritalia ambayo sasa inaitwa Leonardo SPA.

Kamapuni hizo moja kutoka Italia na nyingine Ufaransa zilianza kutengeneza ndege za aina hiyo mwaka 1981 ndege yao ya kwanza aina ya ATR 42-300 ilipata ithibati rasmi mwaka 1985.

Jina la familia ATR 42 linatokana na uwezo wa asili wa ndege hizo kubeba abiria 42, japo kulingana na maboresho na mpangilio mbalimbali idadi hiyo hupungua au kuongezeka.

Uzao wa ATR 42-500 ambayo ndiyo ndege ya Precision Air iliyopata ajali ni uzao wa mwaka 1993 na safari ya kwanza ya ndege hizo ilifanyika mwaka 1994 na kupata kibali cha mamlaka ya usafiri wa Anga ya Uingereza na mwaka mmoja baadaye ufaransa.

Kwa mujibu wa taarifa za mtandaoni ATR 42-500 inaongozwa na marubani wawili, uwezo wake ni kubeba abiria 48 na ina injini mbili za mapanga aina ya PW-127E.

Uwezo wake wa kazi ni Kilometa 554 kwa saa au 299 kts na uwezo wake wa kupaa ni futi 19.7 kutoka usawa wa ardhi, sawa na mita 6,000 au kilometa 6.

Uzani wake ni tani 11.25 na mafuta yake ni tani 4.5 na uwezo wake wa kupakia mzigo ni tani 5.45, jumla ya uzani wake wa kupaa wa mwisho ni tani 18.6 na wa kutua ni 18.3.

Eneo la ndani ya ndege hiyo ni urefu wa mita 13.85, upana mita 2.26 na urefu wa mita 1.91.