Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ITU yabariki Tanzania kuanzisha kituo cha kitaifa cha ubunifu Tehama

Tanzania imepewa nafasi ya kuanzisha kituo cha kitaifa cha ubunifu wa Tehama kitakachosimamiwa na Tume ya Tehama ikiwa ni sehemu ya Mtandao wa vituo vya ubunifu (ITU Acceleration Centres) ambavyo vimegawanywa kwenye ngazi ya Kidunia, Kikanda na Kitaifa.

Hatua hiyo ni mkakati wa ITU kuhakikisha Ubunifu wa Tehama unahusika kuchagiza mapinduzi ya kiuchumi katika nchi wanachama ili kuchagiza ukuaji wa uchumi wa kidijiti.

Akizungumzia Mkutano huo  ambao umefanyika mjini Geneva, Mjumbe wa Bodi hiyo na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dk Jabiri Bakari alisema kItuo hicho kitachochea mabadiliko ya ikolojia nzima ya bunifu za Tehama ndani ya nchi, kikanda na duniani kwa ujumla, pia lengo la mkutano huo ni kuzindua bodi pamoja na kujadili kazi zitakazofanywa na bodi pamoja na kubadilishana uzoefu kwenye masuala ya ubunifu wa kidigiti.  

“Hapa tumeangalia njia za kukuza bunifu mbalimbali za Tehama, kukuza ushirikiano kati ya vyuo vikuu vya ubunifu na taasisi zinazojihusisha na ubunifu, tumeangalia namna tunavyoweza kuwa na mfumo utakaowezesha ubadilishanaji wa taarifa za vituo vya ubunifu duniani, mambo ya haki-miliki za ubunifu, ushirikishwaji wa Serikali katika kukuza ubunifu na vipaumbele katika ubunifu hasa bunifu zinazotatua changamoto za jamii,” alisema Dk Bakari

Bodi ya Wadau wa Usimamizi wa Bunifu (ITU Innovation Board) inaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mawasiliano ya ITU Dk Cosmas Zavazava ambaye ni Mwenyekiti ikiwa na wajumbe 23 ambapo Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dk Bakari ni miongoni mwa wajumbe wa bodi hiyo.  

Pamoja na wajumbe wa nchi nyingine bara la Afrika linawakilishwa na wajumbe nane kutoka nchi za Tanzania, Afrika Kusini, Nigeria, Misri, Kenya, Zimbabwe, Gabon na Malawi.

Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) limeweka bayana kupitia tovuti yake kwamba wajumbe wa Bodi hiyo ikiwemo Tanzania watakuwa chachu muhimu ya kujenga mustakabali jumuishi wa kidijiti kwa watu wote, kwa kuwa ushirikiano huo unalenga kuharakisha mageuzi ya kidijiti kwa kuwezesha ubunifu wa kidijiti na kuchagiza tunu za ujasiriamali kupitia bunifu hizo ambapo uwepo wa Tanzania unaipa fursa nchi kunufaika zaidi na maazimio ya kitaalamu kupitia jukwaa hilo.