Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jaji Mutungi aonya mchakato wa Katiba Mpya

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi

Muktasari:

  • Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi ameshauri kuwepo kwa muda wa kutosha katika mjadala wa Katiba Mpya ili kupata maoni toka makundi mbali mbali kabla ya kuitishwa kwa mkutano maalumu.

Dar es Salaam. Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi ameshauri kuwepo kwa muda wa kutosha katika mjadala wa Katiba Mpya ili kupata maoni toka makundi mbali mbali kabla ya kuitishwa kwa mkutano maalumu.

 Akizungumza jana na runinga ya Azam, Jaji Mutungi amsema  kuna watu wanatamani mkutano maalumu uitishwe kwa haraka, lakini serikali inaepuka hilo kwa sababu wajumbe wanaweza kuja na mawazo yao.

“Tukiitisha mkutano maalumu mapema tunaogopa wajumbe wanaweza kuja na mawazo yao badala ya uwakilishi wa makundi yao, sasa kwa muda uliotolewa kila mtu arudi kwenye kundi lake wajiandae na maoni kuntu ambayo wakija kuwasilisha yataleta  sura nzuri ya Katiba,” amesema Msajili huyo.

Kuhusu wanasiasa Mutungi aliwataka kuheshimu kauli ya Wananchi na waone kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi wa kawaida kushiriki katika mchakato huo, ili kuleta taswira ya wote katika Katiba Mpya.

“Kauli yangu ninayotaka kuwapa wananchi, wanapaswa kuwa wavumilivu na kukubali mchakato unavyoendelea ili itusaidie kufika sehemu ambayo hatutakwama,”Jaji Mutungi amesema.

Hofu ya Msajili huyo wa Vyama vya Siasa nchini imejengeka kwa kile kilichowahi 2014 na hivyo kuwa  kizingiti cha kukwamisha mchakato huo usiendelee, hivyo awaasa wanasiasa kuepuka hali hiyo isijitokeze tena baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuurejesha.

Mutungi ambaye ni mlezi wa Vyama vya Siasa nchini, alissisitiza chochote kinachopangwa kufanyika, umakini unapaswa kuzingatiwa kwa kurejea mapungufu yaliyofanya mchakato wa awali ukakwama.