Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jalada kesi ya wanaodaiwa kuchana noti za BoT, lipo mikononi mwa DPP

Muktasari:

  • Kwa mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Decemba 14, 2020, wakikabiliwa na mashtaka hayo likiwemo la kuharibu noti kwa kuzikatataka zenye thamani ya Sh 4.6 bilioni.

Dar es Salaam. Jalada la kesi ya uhujumu uchumi inayowakabiliwa washtakiwa 13, wakiwemo waliyokuwa watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), lipo mezani kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya kupitiwa na kutolewa maamuzi.


Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka matano, likiwemo la kuharibu noti 4.6 milioni kwa kuzichanachana na hivyo kuisababishia benki hiyo hasara  ya Sh 4.6 bilioni.


Washtakiwa katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 100/2022 ni Mariagoreth Kunzugala maarufu kama Bonge, Henry Mbowe maarufu kama Mzee wa Vichwa, Asha Sekiboko, Cecilia Mpande,  Agripina Komba, Zubeda Mjewa, Khadija Kassunsumo na Mwanaheri Omary wote walikuwa wafanyakazi wa BoT na wakazi wa jijini Dar es Salaam.


Wakili wa Serikali Mwandamizi, Grace Mwanga ameieleza Mahakama ya Kisutu, leo Novemba 9, 2022, wakati shauri hilo lilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.


Mwanga ameieleza Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate, kuwa licha ya upelelezi wa shauri hilo kutokukamilika,  lakini jalada halisi lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Mashtaka kwa ajili ya kulipitia na kulitolea uamuzi.


Hakimu Kabate baada ya kusikiliza maelezo hayo, ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 8, 2022 itakapotajwa na washtakiwa wapo nje kwa dhamana.


Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ambao sio watumishi wa BoT ni Alistides Genand, Musa Chengula, Zaituni Chihipo na Respicius Rutabilwa.


Katika hati ya mashitaka inadaiwa,  kati ya Januari 2017 hadi Septemba 30, 2019, washtakiwa wakiwa Watumishi wa BoT, kwa kuvunja majukumu yao ya kazi waliwezesha utendekaji wa kosa la kuongoza genge la uhalifu.


Pia inadaiwa, Genand, Mchegage, Chengula,  Chihipo na Ishengoma wakiwa si watumishi wa BoT, kwa kushirikiana na watumishi hao wa BoT kwa makusudi, waliwezesha kutendeka kosa la uhalifu wa kupanga.


Katika shitaka la tatu, washtakiwa wote bila ya kuwa na kibali na kutokuwa wazalendo, waliharibu noti 460,000 za Sh10,000 kila moja kwa kuzikatakata zenye thamani ya Sh 4.6 bilioni


Katika shitaka la nne, siku na maeneo hayo, kwa mawasilisho ya kilaghai, kwa kujua na kwa mpango wa kitapeli washitakiwa wote walijipatia faida ya Sh bilioni 1.5 kutoka BoT baada ya kuwasilisha noti hizo BoT.


Katika shitaka la tano washitakiwa wote wanadaiwa kuisababishia BoT hasara ya Sh 4.6 bilioni.


Awali, washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka sita, lakini Juni 18, 2021, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Slyvester Mwakitalu aliwafutia shtaka la kutakatisha fedha na hivyo kubaki na mashtaka matano.


Kwa mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Decemba 14, 2020.