Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jela maisha kwa kulawiti wanafunzi wawili

Muktasari:

Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora imemuhukumu kifungo cha maisha jela Daud Masanja kwa kosa la kulawiti wanafunzi wawili wa shule ya msingi.

Tabora.  Mkazi wa Mtaa wa Masanga Kata ya Igunga mjini Daud Masanja (28) amehukumiwa kifungo cha maisha jela na Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora  kwa kosa la kuwalawiti wanafunzi wawili wa shule ya msingi Azimio.

Adhabu hiyo imetolewa leo Jumatatu Septemba 4, 2023 na Hakimu Mfawidhi wa Wilaya hiyo, Lydia Ilunda baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Awali mwendesha mashtaka wa Serikali, Grace Lwila akimsomea mashitaka mawili ya kulawiti mshtakiwa huyo mbele ya Hakimu Lydia, ameiambia Mahakama kuwa Daudi alitenda makosa hayo Mej 16, 2023 mchana katika Mtaa wa Masanga kata ya Igunga mjini.

Amesema katika tarehe hiyo na muda huo alimlawiti mwanafunzi wa miaka 13 anayesoma darasa  la sita shule ya msingi Azimio, baada ya kumaliza kumlawiti alienda kwa mwanafunzi mwingine wa miaka nane anayesoma darasa la tatu shuleni hapo na kumlawiti na yeye hivyo kuwasababishia maumivu makali.

Mwendesha mashtaka huyo aliendelea kuiambia Mahakama kuwa mshtakiwa Daudi alitenda makosa hayo mawili kinyume na kifungu 154 A cha kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya mwaka 2022 inayozuia kutenda makosa kama hayo.

Hata hivyo baada ya kusomewa mashtaka hayo mawili mshtakiwa huyo alikana kuyatenda na ndipo upande wa Jamhuri ulipopeleka mashahidi nane Mahakamani wakiwemo wanafunzi hao pamoja na daktari ambao kwa nyakati tofauti wote walitoa ushahidi mahakamani wa kumtambua mshtakiwa.

Baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili ambapo mshtakiwa hakuwa na shahidi yoyote, Hakimu Lydia amesema ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri Mahakama imeridhika nao pasipo shaka hivyo, Mahakama imemuona mshtakiwa ana hatia.

Kabla ya Mahakama kutoa adhabu kwa mshitakiwa huyo mwendesha mashitaka wa Serikali, Grace Lwila aliiomba kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa kwa kuwa kitendo alichofanya  ni cha aibu na kimeleta fedheha kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Akitoa hukumu, Hakimu Lydia amesema Mahakama inaungana na upande wa mashtaka hivyo mshtakiwa kwa makosa yote mawili ya kulawiti Mahakama inamuhukumu kutumikia adhabu ya kifungo cha maisha gerezani ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.