Jengo la kihistoria Beit-al-Ajaib laanguka Zanzibar

Jengo laanguka Zanzibar, wanne wahofiwa kufukiwa na kifusi

Muktasari:

Jengo la kihistoria la Beit-al-Ajaib lililopo mji Mkongwe mjini Unguja, Zanzibar lililokuwa likifanyiwa ukarabati limeanguka huku watu kadhaa wakidaiwa kufukiwa na kifusi.

Unguja. Jengo la kihistoria la Beit-al-Ajaib lililopo mji Mkongwe mjini Unguja, Zanzibar lililokuwa likifanyiwa ukarabati limeanguka huku watu kadhaa wakidaiwa kufukiwa na kifusi.

Jitihada za kuwaokoa zinaendelea kufanywa na kikosi maalumu cha huduma za uokoaji.

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amefika eneo la tukio na kupewa taarifa kuhusu uokoaji unaoendelea.

Habari zaidi endelea kufuatilia mtandao wa Mwananchi