Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jokate ataka vijana wasiharakie mafanikio

Katibu Mkuu wa UWT, Jokate Mwegelo akizungumzia kuhusu kongamano la Vijana wakristo wafanyakazi (Viwawa) mjini Tabora leo, kulia ni Makamu wa Askofu Mkuu Padri Faustine Rwechungura. Pcha na Robert Kakwesi

Muktasari:

Baadhi ya vijana wamekuwa wakitaka mafanikio ya haraka pasipo kuwekeza katika mambo ya msingi kama elimu na kazi ambayo  yanachukua muda mrefu.

Tabora. Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jokate Mwegelo amewataka vijana nchini kuachana na ndoto za kupata mafanikio haraka bila kuwekeza kwenye elimu, kazi, jitihada, uvumilivu na hofu ya Mungu.

Akizungumza leo Ijumaa Novemba 24, 2023 kuhusu kongamano la vijana wakristo wafanyakazi (Viwawa) wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora, Jokate amesema uwekezaji huo uchukua muda mrefu.

Amesema kila jambo zuri lina misingi yake na kwamba msingi wa kufanikiwa ni kuwa na uvumilivu sanjali na kuwekeza iwe katika elimu au ufanyaji kazi na hofu ya Mungu.

Katika kongamano hilo ambalo kilele chake ni Novemba 26, 2023 mjini Igunga, Jokate amemtolea mfano Yesu akidai pamoja na uwezo wake alilazimika kusubiri zaidi ya miaka 30 kuanza kufanya kazi yake jambo linalodhihirisha uwekezaji katika kufanya mambo.

"Mafanikio ya haraka pasipo kuwekeza sio jambo rahisi kutokea kama wengi wanavyodhani bali lazima kuwekeza jambo linalochukua muda mrefu na kuhitaji uvumilivu ,"amesema

Huku akisisitiza mafanikio hayaji kwa siku moja, ameliomba kanisa kuwekeza katika imani ili waumini wake waishi kwa imani na sio kusubiri wanapopata tatizo ndio wamkumbuke Mungu.

Makamu wa Askofu Mkuu Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, Padri Faustine Rwechungura amesema vijana ni kundi muhimu ambalo lina nguvu na ndoto za maisha ambazo zisipotekelezwa itakuwa shida na kusababisha kuchukua njia za mkato.

"Tunataka vijana wafahamu wajibu wao katika maisha yao na Taifa kwa ujumla na kuwaeleza kuwa kamwe wasitegemee miujiza kama njia ya mafanikio bali kufanya kazi kwa bidii na kujituma,"amesema

Mratibu wa kongamano hhilo, Peter Kahama amesema vijana 1,200 wanashiriki kongamano hilo ambalo kilele chake misa takatifu itafanyika ikiongozwa na Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa akisaidiwa na Askofu Mkuu mstaafu Jimbo Kuu la Tabora, Paul Ruzoka.

Ameeleza kuwa katika kongamano hilo vijana wanajifunza mambo mengi baadhi ikiwa ni mahusiano, uchumba, ndoa, uongozi, siasa na imani.