Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kada wa CCM aliyehifadhi viatu vya Mandela afariki dunia

Mwenyekiti wa kwanza mwanamke wa CCM afariki dunia

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa kwanza mwanamke wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro, Vick Nsilo Swai, amefariki dunia.

Moshi. Mwenyekiti wa kwanza mwanamke wa CCM Mkoa wa  Kilimanjaro, Vick Swai amefariki dunia.

Vicky aliyekuwa mwenyekiti mwaka 2002 hadi 2012 amefariki dunia jana Jumatatu Mei 31, 2021 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mbali na kuwa mwenyekiti wa CCM,Vick  atakumbukwa kwa kuhifadhi  viatu vya rais wa zamani wa Afrika Kusini,  Hayati  Nelson Mandela.

Mandela aliviacha viatu hivyo mwaka 1962 alipoingia Tanzania kwa mara ya kwanza akitokea Afrika Kusini ili kuanza harakati za ukombozi, lakini kabla ya kuvichukua  alikamatwa na kufungwa gerezani.

Baada ya kutoka gerezani mwaka  1995,   Vick alimkabidhi  Mandela viatu vyake alivyovihifadhi kwa takribani miaka 30.

Akizungumzia kifo hicho  leo Jumanne Juni Mosi,   2021 mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi amesema watamkumbuka kwa ushujaa wake kwa kuwa  haikuwa rahisi mwanamke kushika nafasi hiyo ya juu kwa vipindi viwili.

Boisafi amesema kwa sasa wanasubiri vikao vya familia yake ndipo zipangwe taratibu za mazishi.