Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kagera imewagundua wagonjwa 2,995 wa TB

Muktasari:

  • Mkoa wa Kagera umefanikiwa kuwagundua na kuwaweka kwenye matibabu wagonjwa wa Kifua Kikuu (TB) 2,995 kati ya 3,2000 waliokuwa welengwa kwa mwaka 2021.

  

Bukoba. Mkoa wa Kagera umefanikiwa kuwagundua na kuwaweka kwenye matibabu wagonjwa wa Kifua Kikuu (TB) 2,995 kati ya 3,2000 waliokuwa welengwa kwa mwaka 2021.

Takwimu hizo zimetolewa leo Alhamisi Machi  24,2022 na mtaribu wa kifua kikuu na ukoma Mkoa wa Kagera, Dk Martin Rwabilimbo katika maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani yaliyofanyika kimkoa katika manispaa ya Bukoba.

Dk Rwabilimbo amesema idadi ya kuwagundua wagonjwa wa kifua kikuu sugu imeongezeka kwa sababu ya ukuaji wa Teklonojia katika mkoa huo.

Amesema kuwa kwa mwaka 2015 mgonjwa wa kifua kikuu sugu aligundulika mmoja lakini mwaka 2021 waligundulika wagonjwa 19.

 Kwa upande wake, mgeni rasmi ambaye alikuwa Ofisa Biashara wa Mkoa wa Kagera, Issaya Tendega akisoma taarifa kwa niaba ya Katibu tawala wa mkoa huo,  profesa Faustine Kamuzora amesema kutokana na uwepo wa ugonjwa wa kifua kikuu mkoani hapo ameiomba jamii kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara.