Kamala ampongeza Samia, aahidi ushirikiano
Muktasari:
- Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris ametuma ujumbe wa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mwanamke wa kwanza Tanzania kuwa kiongozi mkuu wa nchi.
Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris ametuma ujumbe wa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mwanamke wa kwanza Tanzania kuwa kiongozi mkuu wa nchi.
Kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Twitter, Kamala ameahidi kushirikiana na Samia kudumisha ushirikiano wa nchi hizo mbili.
“Ninatuma salamu za pongezi na kumtakia kila la kheri Samia Suluhu baada ya kuapishwa kama Rais mpya wa Tanzania, mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo, Marekani inajiandaa kufanya kazi kwa pamoja naye katika kudumisha ushirikiano wa nchi zetu,” amesema Kamala.
Kamala ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo katika historia ya Marekani na aliapishwa Januari 20, 2021 sambamba na Rais Joe Biden.
Samia aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania Machi 19, 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021.