Kamati ya Bunge yapendekeza Lema asimamishwe mikutano mitatu

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akimweleza jambo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakati Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kinga, Haki, Maadili, Madaraka ya Bunge, Emmanuel Mwakasaka akiwasilisha bungeni taarifa ya kamati yake kuhusu shauri dhidi ya Lema la kulidharirisha Bunge, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

  • Leo Alhamisi, Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imewasilisha taarifa yake bungeni baada ya kumhoji mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema na kupendekeza asimamishwe kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge.

Dodoma. Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imependekeza mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kusimamishwa kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge kuanzia tarehe ya azimio hilo.

Baada ya mapendekezo hayo yaliyowasilishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka leo Alhamisi Aprili 4, 2019 wabunge wameanza kujadili hoja hiyo ambayo baada ya kuijadili wabunge watahojiwa kama wanakubali mapendekezo hayo au la.

Wakati wa mjadala huo, wabunge wa Chadema na baadhi ya wabunge wa CUF wametoka nje ya ukumbi wa Bunge.

Lema ameonekana akiwa amekaa akifuatilia mjadala huo pembeni mwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.

Endelea kufuatilia Mwananchi