Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kambi ya Kliniki ya Afya Check, Vodacoma yavuta umati Mwanza

Joyce Albert, Afisa lishe kutoka Kituo cha Afya Buzuruga, Joyce Albert (kushoto) akitoa ushauri kwa baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliojitokeza kupima afya bila malipo katika Kliniki ya Afya iliyoandaliwa na taasisi ya Afya Check kwa kushirikiana na wadau wengine kupitia udhamini wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom. Picha na Mpiga Picha Wetu

Muktasari:

Kambi hiyo ya vipimo na ushauri wa kitaalam inaendeshwa na taasisi ya Afya Check kwa kushirikiana na wadau wengine chini ya udhamini wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.

Mwanza. Mamia ya wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wamejitokeza kupima afya bila malipo kupitia kambi ya kliniki ya afya ya siku mbili inayoendelea katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.

Kambi hiyo ya vipimo na ushauri wa kitaalam inaendeshwa na taasisi ya Afya Check kwa kushirikiana na wadau wengine chini ya udhamini wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 9, 2023 wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo, Dk Isaac Maro kutoka Afya Check amewahimiza wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa inayoundwa na Mwanza, Mara, Geita, Kagera, Simiyu na Shinyanga kujitokeza kwa wingi kupima na kujua afya zao.

‘’Upimaji wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni miongozi mwa huduma zitakazotolewa katika kiliniki hii ya siku mbili; nawasihi wananchi wajitokeze kupima na kujua afya zao ili watakaobainika kuwa na tatizo wapatiwe tiba sahihi mapema,’’ amesema Dk Maro

Ametaja baadhi ya magonjwa yasiyoambukiza ambayo mara nyingi huchelewa kugundulika kutokana na watu wengi kutokuwa na tabia ya kupima afya mara kwa mara kuwa ni pamoja na shinikizo la damu, saratani na uvimbe kwenye mfuko wa kizazi kwa akina mama.

Ali Hassan, mkazi wa eneo la Buhongwa jijini Mwanza ambaye ni kati ya waliojitokeza kupima afya zao amewashukuru wadau kwa huduma hiyo akisema inawezesha watu wasio na uwezo wa kumudu gharama kubwa ya vipimo kupata huduma.

‘’Nimefika hapa asubuhi na tayari nimepata huduma ya kupima afya bila malipo; huduma hii ingenigharimu fedha nyingi iwapo ningelipia. Nawasihi watu wengi wajitokeze kupima afya zao na kupata ushauri wa kitaalam,’’ amesema Hassan

Hoja hiyo imeungwa mkono na Joyadia Halfan, mkazi wa Muleba Mkoa wa Kagera amesema kupitia vipimo alivyopata, anatarajia kufahamu tatizo lake la kiafya la muda mrefu.

‘’Nimeshapita kwenye hospitali kadhaa mkoani Kagera kupima afya bila mafanikio kwa sababu maradhi yangu hayajagundulika; natarajia sasa tatizo langu litagundulika na kupatiwa tiba sahihi,’’ amesema Joyadia