Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kampuni ya Sinotruck kujenga kiwanda cha kuunganisha malori

Muktasari:

Sinotruk ambayo ni miongoni mwa kampuni kubwa za utengenezaji wa malori duniani, tayari inauza bidhaa zake katika nchi zaidi ya 110 inatarajia kujenga kiwanda hicho chenye thamani ya Dola za Kimarekani Sh46.3 bilioni.

Dar es Salaam. Katika jitihada za kuendeleza sekta ya usafirishaji nchini, kampuni ya uuzaji na utengenezaji wa magari ya kusafirisha mizigo kutoka nchini China ya Sinotruk International inatarajia kujenga kiwanda cha kuunganisha malori ili kurahisisha upatikanaji wa magari hayo hapa nchini.

Sinotruk ambayo ni miongoni mwa kampuni kubwa za utengenezaji wa malori duniani, tayari inauza bidhaa zake katika nchi zaidi ya 110 inatarajia kujenga kiwanda hicho chenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 20 (Sh46.3bilioni).

Meneja Mkuu wa kampuni ya Sinotruk International nchini, Li Zhongyuan alisema, “Mwaka 2022, Kampuni za Sinotruk and Saturn Corporation Limited tunatarajia kujenga kiwanda cha uundaji wa vifaa vya malori/magari ya mizigo Tanzania Kiwanda hiki kikianza shughuli zake, kinatarajia kuzalisha ajira takribani 500 kwa Watanzania, na kukuza maendeleo ya sekta ya magari Tanzania."

Wakati kampuni hiyo ikikabidhi malori mapya zaidi ya 100 kwa kampuni ya GSM kupitia kampuni yake ya Usafirishaji ya Galco Limited, Zgongyuan alisema Siku zote Sinotruk inaendesha shughuli zake kwa kuzingatia kuwapatia wateja wake huduma bora na za kisasa, bidhaa na huduma zenye ubora wa hali ya juu, na kwa pamoja kutengeneza mazingira bora kwa vizazi vijavyo.

“Katika Nyanja ya usafirishaji, Sinotruk imefanikiwa kutoa huduma zake na kuanzisha mahusiano ya muda mrefu na kampuni kubwa kama vile GSM, Dangote, OILCOM (T) LIMITED, Tanzania Road Haulage (1980) Limited, Golden Coach/Fleet Ltd, ASAS, AZAM, na Mount Meru. Malori ya HOWO ni mengi mipaka ya nchi, majiji, na vijiji tofauti nchini," alisema.

Kwa sasa Sinotruck inazalisha malori takribani 50,000 ya kusafirisha mizigo na kufanya kazi nzito kwa mwaka na inaongoza kwa viwango kwenye sekta ya magari ya mizigo mizito nchini China kwa miaka 17 mfululizo, kwa Afrika tayari ina viwanda sita vya kuundia, ofisi 26, mawakala 96, na zaidi ya njia 200 za kuwafikia wateja wake kupitia upatikanaji wa vipuli.