Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Katibu wa CCM Rombo afariki dunia akipatiwa matibabu

Katibu wa CCM Wilaya ya Rombo, Marry Sule enzi za uhai wake.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, Marry Sule amefariki dunia jana usiku Machi 18, 2025 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Huruma.

Taarifa za kifo chake zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii usiku huohuo zikieleza kuwa Katibu huyo amefariki muda mfupi baada ya kutoka kwenye chumba cha upasuaji kwenye Hospitali ya Huruma, iliyopo wilayani humo.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rombo, Antony Tesha amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

"Nasikitika kutangaza kifo cha Katibu wa CCM Wilaya,  ndugu Mary Sule kilichotokea jana usiku katika Hospitali ya Huruma alikokuwa akipatiwa matibabu,"imeeleza taarifa hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rombo


Endelea kufuatilia mitandao yetu kwa habari zaidi.