Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kauli ya Polisi wanaohamasisha maandamano Julai 7

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uchunguzi unaofanywa na Jeshi la Polisi kwa saa 24 kupitia mifumo mbalimbali, umebaini baadhi ya watu waliokuwa wakihamasishana kufanya maandamano Julai 7, sasa wanahamasisha vitendo vya kihalifu.

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Tanzania limesema linafuatilia watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuhamasisha vitendo vinavyokiuka sheria, likidai baadhi yao wameacha ajenda ya kuhamasisha maandamano na sasa wanahamasishana kufanya uhalifu utakaohatarisha usalama wa wananchi na mali zao.

Taarifa iliyotolewa leo, Juni 19, 2026, na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, imeeleza kuwa hali ya usalama nchini inaendelea kuwa shwari kutokana na ushirikiano kati ya wananchi, polisi na wadau mbalimbali katika kuzuia na kukabiliana na uhalifu.

Hata hivyo, jeshi hilo limesema siku za karibuni limepokea maswali kutoka kwa wananchi kuhusu hatua zinazochukuliwa dhidi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuhamasisha vitendo vya uvunjifu wa amani.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uchunguzi unaofanywa na Jeshi la Polisi kwa saa 24 kupitia mifumo mbalimbali, umebaini kuwa baadhi ya watu waliokuwa wakihamasishana kufanya maandamano Julai 7 sasa wanahamasisha vitendo vya kihalifu.

"Miongoni mwa vitendo vinavyohamasishwa ni kufunga barabara, kuchoma shule moto ili kusababisha taharuki kwa wazazi na walezi, kushambulia wananchi, kuharibu mali za umma na binafsi, pamoja na kufanya mauaji," imeeleza taarifa hiyo ya Polisi.

Misime amesema kupitia taarifa hiyo kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakihamasishana kuvamia askari wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa lengo la kuwapora silaha na kuzitumia kutekeleza vitendo vya uhalifu.

Jeshi hilo limesema vitendo hivyo haviwezi kuhalalishwa kwa madai ya kutumia haki ya kufanya maandamano ya Amani, kwa kuwa vinakiuka sheria za nchi, misingi ya utawala wa sheria na kuhatarisha usalama wa taifa.

"Hakuna haki ya kuhamasisha vitendo vya kihalifu vinavyolenga kuhatarisha maisha ya watu na mali zao au kuwanyima wananchi uhuru wa kufanya shughuli zao za kila siku," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Polisi imesema inaendelea kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wote wanaohusika na vitendo hivyo huku ikiendelea kuwafuatilia kwa karibu.

"Jeshi la Polisi linawataka wananchi kushirikiana kupinga na kutoa taarifa kuhusu ujumbe wowote unaohamasisha uhalifu badala ya kuusambaza," taarifa hiyo iliyotolewa na Misime imeeleza.

Amesema usalama nchini utaendelea kuimarishwa kupitia ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kudumishwa.