Kaya zilizotaifishiwa mifugo na Serikali zaomba kuingizwa Tasaf
Loliondo. Kaya 17 katika Kijiji cha Mondorosi, Kata ya Soitisambu,Tarafa ya Loliondo Wilaya ya Ngorongoro, ambazo Mifugo yao 220 imetaifishwa na Serikali zimemuomba Rais Samia Suluhu kuzisaidia kuingizwa katika Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf).
Mifugo 220 ya Kaya hizo ni miongoni mwa mifugo 806 ambayo Serikali iliikamata kwa tuhuma za kuingizwa hifadhi ya Serengeti na kuamuliwa kutaifishwa na ilipigwa mnada Oktoba 30 mwaka huu.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Novemba 11, 2023 katika kijiji cha Mondorosi , wananchi hao wameeleza baada ya kukosa mifugo yao maisha yamebadilika na kuwa ya umasikini.
Kiongozi wa Kaya hizo, Amani Ole Lengume amesema kata zao walikuwa na uwezo wa kusomesha watoto, kula na kulipa ada za shule lakini sasa hawawezi tena.
"Tumegeuka masikini, hatuna tena Mifugo ,wamechukua mifugo yote ,hatuna tena maziwa na sisi mifugo ndio tegemeo letu alisema huku akilia,"
Mzee Rapasyo Lengume amesema wanamuomba Rais Samia kuwasaidia kuwaondoa katika umasikini kwani maisha yao yamekuwa magumu sana.
"Tumeambiwa kuna mfukowa Tasaf tunaomba kuingizwa na sisi kupata msaada ili watoto wasirudi nyumbani kutokana na njaa na kukosa ada,"amesema
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Joshua Makko amesema Kata hizo 17 zimegeuka masikini kutokana na kunyang'anywa mifugo yote kwa madai ya uongo kuwa ilikuwa hifadhini.
"Mimi pamoja na madiwani wawili na wenyeviti wa vijiji vya jirani baada ya mifugo kukamatwa tulikwenda kuomba iachiwe kwani ilikuwa inachungwa eneo la Olkimbai nje ya hifadhi na tupo tayari kwa mazungumzo,"amesema
Amesema jitihada zao zilikwama kwani mifugo ya kata hiyo pamoja na mingine.
Sakata la Mifugo ya wananchi hao kufilisiwa na Serikali pia liliwasilishwa bungeni katika hoja binafsi ya Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Oleshangay na Serikali imeahidi kuendelea kulifatilia huku ikikiri kuuzwa Mifugo hiyo kisheria baada ya kuingizwa hifadhini.