Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KIA yapokea wafanyakazi 23 kutoka Microsoft

Watalii kutoka mataifa mbalimbali duniani wakiwemo Wafanyakazi wa Kampuni ya Microsoft kutoka Israel wakitembea baada ya kushuka kwenye ndege ya Ethiopian Airlines katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro(KIA). Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

  • Maboresho yaliyofanyika katika Uwanja Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) na filamu ya ‘Royal Tour’ vimetajwa kama chachu ya kuongezeka kwa idadi ya wageni wanaofika nchini kuamua kutumia uwanja huo.

Hai. Maboresho yaliyofanyika katika Uwanja Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) pamoja na filamu ya ‘Royal Tour,’ vimetajwa kuwa chachu ya ongezeka la wageni (watalii) wanaofika nchini, kuamua kutumia uwanja huo.

Hayo ameyasema leo, Julai 5, 2023 na Mkurugenzi wa Operesheni na Ufundi wa uwanja huo, Martine Kinyamagoha wakati akiwapokea umepokea wafanyakazi 23 kutoka kampuni ya Micriosoft ya nchini Israel, ambao wamefika kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii hapa nchini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, ugeni huo utakaa nchini kwa siku 8 huku ukitembelea vivutio mbali mbali vya utalii ikiwemo hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Ngorongoro pamoja na hifadhi nyingine.

“Msimu wa utalii umeanza na kila siku tunapokea watalii wengi zaidi na haya ni pamoja na matokeo makubwa ya Serikali ya awamu ya sita kutangaza vivutio vyetu vya utalii, lakini pia maboresho ya uwanja wetu, imechangia kuwa na ongezeko hili kitu ambacho sio cha kawaida," amesema na kuongeza;

"KIA kwa viwanja vya Tanzania, kinashika namba moja kwa kuwa na ongezeko kubwa la abiria na hii ni matokea makubwa yanayotokana na filamu ya 'Royal Tour' ambayo imelenga kutangaza vivutio vyetu vya utalii vilivyopo hapa nchini."

Amesema ujio wa wafanyakazi hao wa Microsoft ni jambo kubwa katika nchini na kwamba inaonyesha ni jinsi gani nchi inavyoaminiwa na makampuni makubwa duniani kuja kufanya utalii hapa nchini.

Akizungumzia ugeni huo, Ofisa Mtendaji Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ester Solomoni amesema: "Sasa hivi tunaona makampuni makubwa duniani yameanza kuandaa vifurushi vya utalii ambapo wamechagua Tanzania.”

Aidha amesema kuwa TTB imefurahishwa na kitendo cha kampuni hiyo kuwaleta wafanyakazi wake kuja kutembea kwenye vivutio vyetu vya utalii hapa nchini.

Mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo, Arick Msengi amesema wamechagua kuja Tanzania kwa kuwa ni nchi yenye vivutio vingi vyenye madhari nzuri na utulivu na kwamba watakaa hapa nchini kwa siku 8 wakitembea maeneo mbalimbali.

Naye, mmoja wa wadau wa utalii na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiwoito Afrika Safaris, Charless Mosses, amesema ujio wao ni jambo  la kujivunia na ni fahari kubwa katika nchi, kwa kuaminiwa na Mataifa makubwa.

"Ujio wa wafanyakazi hawa wa Microsoft ambao watatembelea hifadhi za Taifa ni moja ya mpango wa Rais Samia kufikisha watalii milioni 5 ifikapo 2025 na hii ni tunda la safari yake ya 'Royal Tour' ambayo inaendelea,"