Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiama chaja wafanyabiara dawa za kulevya Zanzibar

Kamishna mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa Dawa za Kulevya Zanzibar, Kanali Burhan Zubeir Nassor akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya kupinga dawa za kulevya. Picha na Jesse Mikofu

Unguja. Wakati ikielekea siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupamba na Dawa za Kulevya Zanzibar, imetoa fursa kwa wanaojihusisha na biashara hiyo kujisalimisha kwa hiari au wahame nchi vinginevyo hakuna atakayebaki salama.

Ifikapo Juni 26 kila mwaka dunia huadhimisha siku ya kupiga vita matumizi na usafirishaji haramu wa dawa za kulevya kama ilivyopitishwa katika kikao cha Baraza la Umoja wa Mataifa mwaka 1987.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 24, 2023 Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo, Kanali Burhan Zubeir Nassor amesema uchunguzi wa kutambua mtandao mzima wa uhalifu wa dawa za kulevya unaendelea na kwamba watahakikisha unasambaratishwa.

“Kuna mambo mawili, natoa maagizo wahusika wajisalimishe kwa hiari yao na waache kufanya biashara hiyo au wahame nchi hii maana hakuna atakayebaki salama,” amesema.

Kamishna Burhan amesema ametoa fursa hiyo kwa sasa badala ya kupambana nao lakini atakayeipoteza hataipata tena na atajuta kufanya hivyo.

Amesema iwapo mtu akijisalimisha watakaa na kamati yake kujadili jinsi ya kumtoa mhusika kwenye kundi la uhalifu.

“Baada ya kujisamilisha tutafanya uchunguzi na kupepeleza kwa umakini kuhakikisha unakuwa katika mikono salama lakini ambaye hatajisalimisha atakumbana na mkono wa sheria,” amesema.

Kuhusu changamoto amesema kwasasa sheria inawataka wawe na mashahidi huru lakini watu wanakuwa na muhali kujitokeza kutoa ushahidi.

“Tumeanza kupata shida kidogo hadi masheha wanabadilika kesi imeshafika mahakamani, hii ni changamoto kubwa tunayokumbana nayo lakini sasa tunajipanga kubadili vipengele ambavyo vinaleta changamoto ili sheria isimame vyema katika kupambana na dawa hizo,” amesema.

Uhalifu wa dawa kulevya ni uhalifu mkubwa sana duniani kwasababu wanatumia nguvu kubwa ya kiakili na kifedha huku baadhi ya mataifa au makundi hayo hutumia nguvu ya kijeshi.

Amesema taasisi itaanza kuelimisha wanafunzi wa shule za msing na sekondari na tayari kuna mabalozi watakuwa wanajaza dodoso la tathmini ya elimu ya dawa za kulevya katika kila shule.

Mmoja wa watumiaji wa dawa za kulevya, Shaibu Hussein amesema iwapo wakishirikisha watu wanaoacha kutumia dawa hizo ni rashi kfanikiwa kujua wanaojishusiaha na daw ahizo lakini wamekuwa wkipuuzwa.