Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kichwa cha treni ya umeme chawasili nchini

Kichwa kipya cha treni ya umeme  kilichoundwa na Kampuni ya ‘’Hyundai Rotem (HRC) kimewasili nchini kutokea Korea ya Kusini leo Novemba 2, 2023

Muktasari:

  • Kichwa kimoja cha treni ya kisasa kati ya 17 vilivyokuwa vinategenezwa nchini Korea ya Kisini kimewasili nchini na majaribio yake yanatarajiwa kufanyika baada ya kumaliza ukaguzi wa kichwa na mafunzo ya uendeshaji kwa madereva mapema mwezi Desemba mwaka huu.

Dar es Salaam. Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema kichwa kipya cha treni ya umeme  kilichoundwa na Kampuni ya ‘’Hyundai Rotem (HRC) kimewasili nchini kutokea Korea ya Kusini.

Huku vichwa vingine vitatu kati ya 17 vilivyoagizwa na TRC kutoka kwenye kampuni hiyo vinatarajiwa kupokewa Desemba mwaka huu.

Mfumo unaotumika katika uendeshwaji wa kichwa hicho ni nishati ya umeme wenye msongo wa kilovoti 25 na kitakuwa na nguvu ya kilowati 5,000 sawa na nguvu ya 6,800 kwa kipimo cha House Power.

Kwa mujibu wa Tarifa iliyotolewa kwa umma na taasisi hiyo kupitia kwa Mkuu wa kitengo cha Uhusiano, Jamila Mbarouk amesema  vichwa vilivyobakia mpango wa uletaji na vitendea kazi utakuwa unatekelezwa kwa awamu pindi uundwaji wake utakapokamilika.

 “kichwa kilicholetwa kitakuwa na mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa. Kitakuwa na uwezo wa kuvuta na kulisha umeme kwenye mabehewa yasiyozidi 14 ya  abiria kwa wakati mmoja,”amesema.

Jamila amesema taasisi hiyo inatarajiwa kufanya majaribio ya kichwa cha treni kitakachotumika katika reli ya kiwango cha  kimataifa, kati ya Dar es Salaam hadi Morogoro na baadaye Dar es Salaam hadi jijini Dodoma, baada ya kumaliza ukaguzi wa kichwa na mafunzo ya uendeshaji kwa madereva mapema mwezi Desemba mwaka huu.

Amesema Desemba mwaka huu, TRC inatarajiwa kupokea vichwa vingine vitatu, mpango wa uletaji na vitendea kazi utakuwa unatekelezwa kwa awamu pindi uundwaji wake utakapokamilika.

“TRC imeshapokea mabehewa 35 kwa ajili ya uendeshaji kwa ajili ya uendeshaji wa reli ya kisasa ya (SGR),”amesema.

Kufikia Septemba 2023, mradi wa SGR kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ulifikia silimia 98.6, Morogoro Makutupora umefikia asilimia 95.41, Makutupora –Tabora umefikia asilimia 12.32,Tabora –Isaka asilimia 5.02.

“Mkandarasi kampuni ya CCECC, yupo eneo la mradi  awamu ya pili Tabora-Kigoma,”amesema.