Kigogo ACT Wazalendo afariki dunia
Muktasari:
- Taarifa ya kifo chake imetolewa na mwenyekiti wa chama hicho, Othman Masoud Othman, imeeleza kuwa Gumsani alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Ngome ya Wazee Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo, Yasin Mohamed Gumsani amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatatu Novemba 4, 2024 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa ya kifo chake imetolewa na mwenyekiti wa chama hicho, Othman Masoud Othman, imeeleza kuwa Gumsani alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Amesema taratibu za maziko zitatolewa baadaye.
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi