Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikogwe aliyefunga ndoa akiwa na miaka 102 afariki

Baadhi ya ndugu na jamaa wakiwa nyumbani Kwa marehemu Masasila Kibuta Kijiji cha Nyamazugo Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza. Picha na Daniel Makaka

Muktasari:

Kibuta na mke wake waliingia kwenye historia ya wenza wenye umri mkubwa kufunga pingu za maisha katika Kanisa Katoriki Kigango cha Nyamazungo Parokia ya Ngomamtiba Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Juni 17, mwaka huu

Sengerema. Kikongwe Masasila Kibuta (102) aliyezua gumzo baada ya kufunga ndoa na Chem Malaya (90) wakiwa na umri mkubwa, amefariki dunia leo Agosti 15, 2023 zikiwa ni siku 60 baada ya kufunga pingu za maisha na mpendwa wake.

Kibuta na mke wake waliingia kwenye historia ya wenza wenye umri mkubwa kufunga pingu za maisha katika Kanisa Katoliki Kigango cha Nyamazungo Parokia ya Ngomamtiba Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Juni 17, mwaka huu

Kwa mujibu wa mtoto wake, Alphonce Masasila amesema baba yake amefariki leo Agosti 15, 2023 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Taarifa kutoka ofisi ya Muuguzi Mkuu wa Hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema, zimesema Mzee Kibuta alipokelewa hospitalini hapo Agosti 11, mwaka huu akisumbuliwa na magonjwa mbalimbali na Agosti 15, 2023 saa 12:04 alfajiri akapoteza maisha huku chanzo cha kifo chake kikitajwa kuwa ni Malaria na Figo zake kushindwa kufanya kazi.

Mtoto wa marehemu, Alphonce Masasila amesema mazishi ya yatafanyika Agosti 18, 2023 nyumbani kwake Kijiji cha Nyamazugo wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza.

Enzi za uhai wake baada ya kufunga ndoa, Masasila  alisema amefunga ndoa hiyo ili siku akitoka duniani akaonane na Mungu baada ya kutimiza agano la ndoa takatifu.