Kilichojiri mahakamani kesi ya kina Mbowe hiki hapa…

Muktasari:

  • Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imeahirisha kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu mpaka Alhamisi Januari 13, 2022.

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imeahirisha kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu mpaka Alhamisi Januari 13, 2022.

SOMA:Kilichojiri mahakamani kesi ya kina Mbowe hiki hapa…
Jaji Joachim Tiganga anayeyesikiliza kesi hiyo ameihirisha baada ya shahidi wa nane wa upande mashtaka, Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Wilaya (OC-CID) Arumeru, Mrakibu wa Polisi (SP), Jumanne Malangahe kumaliza ushahidi na kuhojiwa na upande wa utetezi.


Upande wa utetezi walianza jana Jumatatu Januari 10, 2022 kumuhoji shahidi huyo na ukamuomba Jaji kuahirisha kesi hiyo ili kuendelea leo kwa kuwa muda ulikuwa umeshaenda huku upande huo ukidai kuwa bado ulikuwa na maswali mengi mengi.


Leo asubuhi Wakili wa upande wa utetezi Peter Kibatala alianza kumhoji shahidi huyo mpaka mchana ambapo baada ya kumaliza upande wa mashtaka walimuomba Jaji aahirishe kesi kwa kuwa hawakumuandaa shahidi mwingine wa kutoa ushahidi kwa leo.


Baada ya ombi hilo Jaji Tiganga aliwahoji upande wa utetezi ambao uliridhia ombi hilo na kumfanya Jaji kuahirisha kesi hiyo mpaka Alhamisi ambapo shahidi mwingine upande wa mashtaka atafika mahakamani hapo kuanza ushahidi.

Sehemu ya mahojiano kati ya mawakili na shahidi wa nane upande wa mashtaka hii hapa…
Jaji Tiganga ameshaingia na mawakili wa pande zote wanajitambulisha.


Wakili wa utetezi Peter Kibatala anaendelea kumuhoji Shahidi.


Wakili: Katika ushahidi wako kuna mahali Umemzungumzia urio kushiriki katika kutafuta watatu wa kufanya vitendo vya kigaidi


Shahidi: Sijazungumzia.


Wakili: Kwa ufahamu wako uongozi wa Jeshi unafahamu Urio alichokuwa akifanya


Shahidi: Sifahamu


Wakili: Tunakubaliana vitendo vya kigaidi ni vizito na vinatikisa usalama wa nchi


Shahidi: Nafahamu
Wakili: Unafahamu jeshini kuna kitengo kinachochunguza mambo ya kigaidi


Shahidi: Sifahamu


Wakili: Uliieleza kama mlishirikisha vyombo vingine vya kiusalama ikiwemo TISS


Shahidi: Binafsi sikufanya labda viongozi wenzangu


Wakili: Na katika maelezo yako hakuna mahali uliieleza kama mlishirikisha vyombo vingine


Shahidi: Sikueleza


Wakili: Unafahamu kama vyombo vingine vingeshirikishwa taasisi kama idara ya uhamiaji wangeusishwa


Shahidi: Nafahamu


Wakili: Unafahamu shahdi wa nne ndio aliyepanga mpango wote na alidafiri mara kadhaa kwenda nje ya nchi.


Shahidi: Sifahamu


Wakili: Unafahamu Rais Samia alipata wapi taarifa hadi kuwatangazia umma kuwa Mbowe alitoroka nchini


Shahidi: Sifahamu


Wakili: Ni kweli Mbowe alikimbia nchi kukwepa upelelezi


Shahidi: Sifahamu


Wakaili: Ukiwa kama mpelelezi kuna mtu aliwahi kufungiwa kutokana na tuhuma hizi za kigaidi


Shahidi: Siwezi kulizungumzia


Wakili: Kwa ufahamu wako kuliwahi kuwekwa zuio la Mbowe kutotoka nje ya nchi kutokana na tuhuma za kigaidi


Shahidi: Sifahamu


Wakili: Unafahamu kama miamala za kiuchunguzi ziliwasiliana na nchi ambazo Mbowe alitembelea


Shahidi: Sifahamu


Wakili: Agosti 4th 2020 ulijulishwa Mbowe alikuwa akishiriki kula njama za kutenda ugaidi kwanini kipindi chote Mbowe hakukamatwa


Shahidi: Kulikuwa na mambo mengi ya kiupelelezi


Wakili: Kingine mlichokuwa mnachunguza kwa mwaka mzima


Shahidi: Mambo mengi siwezi kuyazungumzia


Wakili: Mambo gani hayo


Shahidi: Mambo mengi ikiwemo wahalifu wengine


Wakili: Ni watu gani hao na wako wapi hapa mahakamani


Shahidi: Waliachiwa


Wakili: Niambie ni watu gani kama sio kumvizia Mbowe akiwa anaatetea Katiba mpya


Wakili: Unafahamu nchi nyingi za kidikteta ni kuwakamata wapinzani na kuwapa kesi za kigaidi


Shahidi: Sifahamu


Wakili: Unafahamu maana ya trevalla advisor


Shahidi: Sijawahi kukutana na kitu kama hicho


Wakili: Uliwahi kusikia tahadhari yoyote iliyotolewa kwenye mikusanyiko baada ya 2020


Shahidi: Sijasikia


Wakili: Katika upelelezi wenu Urio ndio alikuwa informer wenu


Shahidi: Ni sahihi


Wakili: Na wewe ulikuwa unafanya kazi kufuatana na sheria


Shahidi: Ni sahihi


Wakili: Unafahamu Sheri ya kulinda mtoa taarifa


Shahidi: Sifahamu


Wakili: Hata hufahamu kwa mujibu wa mtoa taarifa anapokuja kutoa taarifa mnatakaiwa kumuandikisha maelezo


Shahidi: Sifahamu


Wakili: Kwa upelelezi wako Mbowe aliwahi kuwapa hawa vijana fedha ya kutoka Morogoro kwenda Moshi


Shahidi: Kwa maelezo ya Ling'wenya zilipitia kwa Urio


Wakili: Nitafutie sehemu imeandikwa kuwa pesa zilitumwa kwa Urio kwenda kwa Ling'wenya


Wakili: Wakati fedha zinatumwa Ling'wenya alikuwa anajua rohoni mwake na kwenye fikra zake alikuwa anaenda kufanya kazi ya VIP protection


Shahidi: Sifahamu kwenye fikra zake


Wakili: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama Ling'wenya alikuwa anajua ni nini anaenda kufanya nini


Shahidi: VIP protection


Wkili: Nionyeshe ni wapi Urio alimwambia Ling'wenya kuwa anaenda kufanya kazi ya ugaidi


Shahidi: Hajaonyesha wazi


Wakili: Ni wapi katika maelezo hayo Ling'wenya anakairi alipewa fedha na Mbowe kwenda kufanya vitendo vya kigaidi


Shahidi: Hakuna


Wakili: Mwambie Mheshimiwa Jaji nini kilichowanyima kumpa

vifaa kama kinasa sauti ili kumsikia Mbowe akipanga vitendo vya kigaidi


Shahidi: Siwezi kulizungumzia hilo


Wakili: Tunakubaliana kuwa hatuna hizo sauti


Shahidi: Kwa nafasi yangu hamna hizo sauti


Wakili: Tuna video au hatuna


Shahidi: Hatuna


Wakili: Mliwahi kumwambia Urio anapoongea na Mbowe aweke kinasa sauti


Shahidi: Sikuwahi kukutana na Urio


Wakili: Mliwahi kuwaza kumpeleka polisi wakati Mbowe anatafuta vijana ajifanye nni mmojawapo ili a rekodi


Shahidi: Siwezi kueleza


Wakili: Umefahamu lini kama Urio ni mtoa taarifa wenu


Shahidi: Nlifahamu kati ya mwezi wa nane au watisa


Wakili: Ulishiriki kumkamata Tito Magoti


Shahidi: Sikushiriki


Wakili: Unaugomvi na Tito Magot


Shahidi. Hapana


Wakili: Mwambie Mheshimiwa Jaji cheti ulichotakiwa kukileta kama unacho


Shahidi: Nlieleza jana


Wakili: Unacho


Shahidi: Sina


Wakili: Ni wapi Ling'wenya alikiri kushiriki vikao vya kigaidi


Shahidi: Hakuna


Wakili: Nitafutie Mahali Ling'wenya akieleza bastola itakavyotumika kwenye vitendo vya kigaidi


Shahidi: Hakuna


Wakili: Nionyeshe ni wapi Ling'wenya alieleza vilipuzi vitavyotumika kulipua vituo vya mafuta


Shahidi: Hakuna


Wakili: Hebu niambie pale Rau madukani uwepo wao ulikuwa unahusiana kupanga kutekeleza vitendo vya kigaidi?


Shahidi: Walikuwa kwenye mpango huo


Wakili:Unafahamu Adamoo hii bastola na risasi alipata wapi


Shahidi: Sifahamu


Wakili: Madawa ya kulevya aliyokutwa nayo Ling'wenya mlichinguza amepata wapi


Shahidi: Hatukuchunguza


Wakili: Kwanini hajazungumzia kwenye kesi hii


Shahidi: Hatukuzingumzia


Wakili: Katika uchunguzi wenu mligindua yanahusika vipi na hii kesi


Shahidi: Hatukugundua


Wakili: Nlisika jana ukisema uaskari unashibishwa na kumbukumbu


Shahidi: Kumbukumbu ni moja ya sifa ya askari


Wakili: Ni sahihi Chadema ilijipanga na kushiriki uchaguzi wa mwaka 2020


Shahidi: Ni sahihi


Wakili: Na Mbowe aligombea Ubunge Hai na Tundu Lissu aligombea Urais


Shahidi: Ni sahihi


Wakili: Inakuingia akilini mtu agombee halafu wakati huo akatishe wananchi wanaoenda kumchagua


Shahidi: Siwezi kuongelea hilo


Kibatala: Unafahamu nyumba na namba aliyokuwa anaishi dada yake Ling'wenya?


Shahidi: Sifahamu.


Wakili: Unafahamu Lujenjwe alikuwa anakaa hoteli gani? Nitajie hata moja.


Shahidi: Sifahamu


Kibatala: Nitajie hata moja.


Shahidi: Alikuwa anakaa hoteli mbalimbali


Kibatala: Mheshimiwa Jaji Mimi nafikiri nimemaliza kumuuliza shahidi maswali.


Kwa Sasa amenyanyuka Wakili wa Serikali Mwandamizi Robert Kidando, kwa ajili ya kumuuliza maswali shahidi kukusiana na maswali aliyohijiwa na mawakili wa utetezi kuanzia jana hadi leo
SP Jumanne anafanyiwa cross examination na wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando


SSA Kidando: Shahidi uliulizwa swali na wakili wa utetezi, kama ACP Kingai kama alikuwepo Agosti 9, 2020 kituo cha Polisi Mbweni na wewe ukasema hakuwepo elezea kwanini ulisema hakuwepo?


Shahidi: Tarehe hiyo ACP Kingai hakuwepo kituo cha Polisi Mbeni kwa sababu alikuwa kwenye kazi ya ufuatilia wengine.


Kidando: Uliulizwa kuhusiana na kukamatwa kwa Gabriel Mhina Agosti 19, 2020 na kufikishwa mahakamani Sepemba 31, 2020.


Shahidi: Alichelewa kufikishwa Mahakama katika tarehe hiyo kutokana na shughuli za kipelelezi.


Kidando: Mbowe alikamatwa kwa tuhuma zipi?
Shahidi: Kwa tuhuma za kigaidi na sio za kikatiba.


Kidando: Uliulizwa swali kuhusiana na mshtakiwa wa tatu (Ling'wenya) kufanya kazi ya VIP Protection na ukasema sio kosa kama mtu atafanya kwa nia njema na malengo mema, hapa ulikuwa inamanisha Nini?


Shahidi: Nilisema kufanya kazi ya VIP Protection sio kosa, kama mtu atafanya kwa nia njema lakini kama àtafanya kwa nia ovu hapo ndio kosa.


SSA Kidando: Uliulizwa swali na wakili wa utetezi Dickson Matata kuwa kutumiwa nauli ni kosa au sio kosa na wewe ukasema sio kosa, kwanini ulisema sio kosa?


Shahidi: Sio kosa kama mtu atatumiwa kwa nia njema.


Kidando: SP Jumanne Uliulizwa siku ulipowakamata mshtakiwa wa pili na watatu kule Moshi na kuwafikisha kituo Kikuu cha Polisi Moshi na kuhusiana na kuandikwa katika kitabu cha Kumbukumbu cha mahabusu( Ditention Register- DR)na ukasema mshtakiwa hawakuandikishwa katika kitabu hicho, hapo ulimaanisha Nini?


Shahidi: Mtuhumiwa au watuhumiwa wanaandikwa katika kitabu hicho pale tu anapokuwa ameshikiliwa na kuwekwa mahabusu ndio anaweza kuandikwa kwenye kitabu hicho (DR)


Kidando: Ulizwa swali katika bastola uliyoikamata kwa mshtakiwa wa Pili, kulikuwa na maeneo ambayo yangeweza kutoa alama za vidole ukasema ni kweli na ukasema ushahidi huo wa alama za vidole hukuleta Mahakama, hebu elezea kwanini ushahidi huo hukuleta Mahakama.


Shahidi: Utambuzi wa alama za vidole sikuleta mahakamani kwa sababu haukuwa na umuhimu wa kulinganisha nani alikuwa na hiyo silaha kwa sababu ilikamatwa kwa mshtakiwa huyo na hatukuwa na mashaka na kwamba utambuzi wa alama za vidole( Fingerprint) hufanyika kama tuna mashaka na mtu ndio huwa tunafanya   ulinganishi.


Kidando: Mheshimiwa Jaji kwa upande wa mashtaka hatuna maswali mengine.
Baada ya wakili Kidando kumaliza Re- examination In chief. shahidi wa nane ( SP Jumanne)  kwa sasa anahojiwa tena na wakili Kibatala.


Jaji: Haya maswali mawili uliyoomba Kitabala.
Kibatala: Naomba nipatiwe kielelezo namba 2 na naomba unisomee.


Shahadi anasoma


Kibataka: Hapo ofisa huyo wa Polisi amesaini maelezo hayo au ameandika namba za cheo chake?


Shahidi: Amesaini


Kibatala: Huyo ofisa wa Polisi ni rank 5 au laa?
Shahidi: Ni rank 5


Kibatala: Mheshimiwa sina swali


Jaji: Baada ya kumaliza cross examination, upande wa mashtaka mnakitu cha kumuuliza shahidi?


Kidando: Hatuna cha kumuuliza.


Jaji: Kwa hiyo mmemalizana na shahidi sio?


Kidando: Ndio Mheshimiwa Jaji.


Jaji: Shahidi tunakushukuru kwa uvumilivu wako.


Kidando: Mheshimiwa Jaji, huyo ndio shahidi tuliyokuwa naye kwa leo hivyo tunaomba ahirisho la kesi hii ili tuje tuweze kuendelea kesho kutwa Alhamisi tarehe 13 mwezi wa kwanza mwaka 2022 ambapo tutaketa shahidi mwingine kwa ajili ya kuendelea na shahidi na pamoja ni kwamba saa Saba mchana hatukuweza kuleta shahidi mwingine kwa sababu hatukujua shahidi huyu angeweza kumaliza saa ngapi.
Hivyo tunaomba ahirishwa kwa sababu kesho ni holiday (Sikukuuu).


Jaji: Upande wa utetezi?


Kibatala: Hatuna pingamizi juu ya alichosema Wakili Kidando.


Jaji: Maombi ya upande wa mashtaka yamekubaliwa, hivyo

Jaji: Naahirisha kesi hii Hadi siku ya Alhamisi Januari 13, 2022 itakapokuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi, hivyo naelekeza upande wa mashtaka walete mashahidi na washtakiwa wataendelea kuwa chini ya usimamizi wa mahabusu.
Mchana mwema.