Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kilimanjaro kuchanja polio watoto 287,525

Mratibu wa chanjo Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Peter Kihamia akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

Kutokana na tishio jipya la mlipuko wa ugonjwa wa polio, Mkoa wa Kilimanjaro umejipanga kukabiliana na tishio hilo kwa kuchanja kiasi cha watoto 287,525 wenye umri chini ya miaka mitano.

Moshi. Kutokana na tishio jipya la mlipuko wa ugonjwa wa polio, Mkoa wa Kilimanjaro umejipanga kukabiliana na tishio hilo kwa kuchanja kiasi cha watoto 287,525 wenye umri chini ya miaka mitano.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), ugonjwa wa polio umeripotiwa kulipuka upya nchini Malawi Februari mwaka huu, baada ya shirika hilo kutangaza Agosti 2020 kwamba bara la Afrika halikuwa tena na ugonjwa huo.

Tanzania na Malawi zimepakana kijiografia na raia wake wanamwingiliano wa kila siku, hivyo tahadhari ya chanjo dhidi ya polio ni muhimu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 26, Mratibu wa chanjo Mkoani humo, Dk Peter Kihamia amesema kazi hiyo itafanyika nyumba kwa nyumba kuanzia  Aprili 28 hadi Mei Mosi mwaka huu na timu ya wataalam wapato 626 ambao watafanya kazi hiyo.

"Tunachofanya sasa hivi ni kuimarisha kinga za watoto na kampeni hii ya chanjo itafanyika kwa mizunguko minne, ili kuhakikisha ugonjwa huu tunaudhibiti usiingie kwenye maeneo yetu.

"Ugonjwa huu wa polio ni tishio kwa miaka mingi kama mtakumbuka miaka mingi ya nyuma watu walikuwa wakipata shida ya ugonjwa wa polio na ulikuwa ukisababishwa na virusi vya polio ambao wapo katika makundi matatu," amesema.

Alisema kazi hiyo itaanza Aprili 28 hadi Mei Mosi mwaka huu na kipindi hiki cha siku nne, ambapo watakuwa wakitembea nyumba kwa nyumba mkoa mzima wa Kilimanjaro ili kuwafikia watoto 287,525.

"Kutakuwa na timu za wachanjaji 628 kwa Mkoa mzima wa kilimanjaro na hizi timu zimegawanyika katika makundi mbalimbali na timu moja inakuwa na watu watatu wakiwemo wataalam wa afya," amesema. 

Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Erick Atugonza, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi na kuwataka kutoa ushirikiano na kuhakikisha kila nyumba yenye mtoto chini ya miaka mitano anapata chanjo hiyo.

"Katika kampeni hii hatutaacha mtoto hata mmoja ni lazima watoto wote wapatiwe hii chanjo ya polio na tutapita nyumba kwa nyumba kuhakikisha tunafanya jambo hili kwa ufanisi mkubwa," amesema.