Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kilimanjaro yakabiliwa na ukame, upungufu wa chakula

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai

Muktasari:

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai ametoa rai kwa wananchi kutunza chakula walichonacho ili kukabiliana na athari za ukame zinazoweza kujitokeza.

Siha. Mkoa wa Kilimanjaro unakabiliwa na changamoto ya ukame, hali ambayo imetajwa kuchangia upungufu wa tani 132,584 za chakula.

Hayo yamebainishwa leo Julai 16, 2022 na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai wakati akitoa taarifa kwa makamu wa Rais, Dk Philip Mpango kwenye hafla ya ufunguzi wa maabara ya afya ya jamii ngazi ya tatu ya usalama ya kibaiolojia (BSL3) ya Kibong’oto iliyopo wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.

Amesema hali hiyo imetokana na upungufu wa mvua katika kipindi cha vuli na masika na hivyo kusababisha kushindwa kufikia tani 530,339 za chakula ambazo ni mahitaji ya mkoa kwa mwaka.

“Mkoa wetu huwa una kawaida ya kupata mvua mara mbili, msimu wa vuli na masika lakini mwaka huu tumeambulia kukosa na kutokana na upungufu wa mvua kwa msimu wa mwaka 2021/2022, kuna uwezekano wa kuwa na upungufu wa chakula tani 132,584 kwa mwaka huu 2022/2023,” amesema Kagaigai.

Kufuatia hali hiyo, ametoa rai kwa wananchi kutunza chakula walichonacho ili kukabiliana na athari za ukame zinazoweza kujitokeza.

“Napenda kusisitiza, kila aliye na ziada atunze vizuri chakula alichonacho kwa sababu hatujui yajayo yatakuwaje, amesema RC Kagaigai.