Kina Mbowe kujitetea leo

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu leo wanatarajiwa kuanza kujitetea dhidi ya mashtaka ya ugaidi yanayowakabili.


Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu leo wanatarajiwa kuanza kujitetea dhidi ya mashtaka ya ugaidi yanayowakabili.

Hatua hii ni baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi baada ya kuita mashahidi 13 na Mahakama Kuu (Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi) kuwakuta na kesi ya kujibu. Utetezi wa Mbowe na wenzake - Halfani Hassan, Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya - wanaoshtakiwa kupanga kulipua vituo vya mafuta na maeneo ya mikusanyiko ya watu kama masoko kwa lengo la kuifanya nchi isitawalike unasubiriwa kwa shauku kubwa na watu wengi.

Bwire, Kasekwa na Ling’wenya walikuwa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) JWTZ katika kikosi cha makomando kilichopo Sangasanga, mkoani Morogoro ambao wanadaiwa kuachishwa kazi kwa nyakati tofauti kwa sababu za kinidhamu. Kwa mujibu wa sheria za jinai Tanzania, upande wa mashtaka ndio wenye jukumu la kuthibitisha kosa dhidi ya washtakiwa bila kuacha mashaka yoyote, hivyo mashaka yatakayoibuliwa na ushahidi wa kina Mbowe dhidi ya ushahidi wa Jamhuri yatageuka kuwa faida kwa washtakiwa hao.

Mbowe na wenzake wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama kutenda vitendo vya kigaidi, kufadhili vitendo vya kigaidi (Mbowe peke yake); kushiriki vikao vya kutenda vitendo vya kigaidi (wote) na kukutwa na vifaa na bastola ya kutekeleza vitendo vya ugaidi waliyodaiwa kutenda nyakati na mahali tofauti kati ya Mei Mosi na Agosti 5, 2020 katika mikoa ya Morogoro, Kilimanjaro na Dar es Salaam.

Mbowe na wenzake wana kesi ya kujibu

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imewakuta Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu na kesi ya kujibu katika kesi ya ugaidi inayowakabili. Soma zaidi

Kwa nini mashahidi 11 kesi ya kina Mbowe hawakuonekana?

Wakati kesho Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ikitarajiwa kuamua kama Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu wana kesi ya kujibu ama la katika tuhuma za ugaidi zinazowakabili, wataalamu wa masuala ya sheria wamezungumziakutotokea kwa mashahidi 11 wa upande wa mashtaka kutoa usahidi wao katika kesi hiyo. Soma zaidi