Kiongozi Mbio za Mwenge achukizwa kuchelewa ujenzi ofisi za halmashauri

Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, Abdallah Shaibu Kaimu,

Muktasari:

  • Mkimbiza Mwenge Kitaifa, Abdallah Shaibu Kaimu achukizwa na ucheweleshwaji wa ujenzi wa jengo la ofisi za halmashauri.

Ludewa. Abdallah Shaibu Kaimu, Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa achukizwa na kasi ya ujenzi wa jengo la ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.

Amebainisha hayo baada ya ukaguzi wa jengo hilo na kuwataka wataalamu kuwa na uzalendo kwenye kila idara.

“Wataalamu vaeni uzalendo basi haipendezi kuona mzalendo mzima unafanya kazi chini ya kiwango kwakuwa fedha zinazotumika ni za wananchi,” amesema Kaimu

Pia amemwagiza Mkuu wa Wilaya kuhakikisha ujenzi wa jengo hilo unakamika tarehe husika kama alivyo ainisha mkandarasi.

“ Mwenge wa uhuru unaagiza mradi ukamilike kwa wakati, ukamilike tarehe 8/7/2023, Mkuu wa Wilaya kwa nafasi yako wafuatile kwa ukaribu kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati,” amesema Shaibu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyo somwa na mkandarasi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Buteye Jirara imeainisha kuwa kuwa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 78  na matarajio ni kukamilika Julai 8, mwaka huu.

Ameongeza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa imekuwa ikitumia baadhi ya vyumba kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

“ Halmashauri yetu haina ofisi imekuwa ikitumia baadhi ya vyumba vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya kutoka wilaya hii iundwe kwa kuona hilo serikali ili panga kutekeleza ujenzi kwa gharama ya Sh2.8 bilioni ambapo mpaka sasa tumepokea Sh2.65 bilioni huku Sh1.72 bilioni kati ya hizo zikiwa zimetumika,” amesema Jirara.