Kocha Everton alazimisha kujua kiingereza

Marco Silva

Muktasari:

Silva amekaa Uingereza miezi 18

Liverpool, England. Kocha mpya wa klabu ya Everton, Marco Silva, raia wa Ureno, ametoa mpya baada ya kuweka sheria tata ya kumtaka kila mchezaji wake kujuwa kiingereza.

Silva aliyetua Goodison Park hivi karibuni akitokea Watford, amesema inakuwa vigumu kuwanoa wachezaji wasiojua kuzungumza kiingereza.

Kocha huyo alisema lugha inayotumikia kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha klabu hiyo ni kiingereza hivyo mchezaji yeyote wa kigeni aliyesajiliwa au anayetaka kusajiliwa na klabu hiyo ni lazima ajue lugha hiyo.

Tayari Silva amekaa Uingereza miezi 18 lakini ameingia tuisheni na sasa anazungumza kiingereza fasaha pamoja wasaidizi wake Joao Pedro na kocha wa viungo Pedro Conceciao ambao pia ni wareno.

Kocha huyo ameanza kazi hiyo na mchezaji wake mpya winga Richarlison raia wa Brazil aliyehama naye kutoka Watford ambaye alifunga mabao mawili katika mechi ya ugenini waliyotoka sare ya 2-2 dhidi ya Wolverhampton Wanderers wiki iliyopita.

Mchezzai mwingine aliyekumbana na kadhia hiyo ya kutakiwa kujua kwanza kiingereza kabla ya kuanza kuitumikia Everton ni mlinzi mpya wa Yerry Mina raia wa Colombia aliyesajiliwa kutoka Barcelona.