Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Koo tano zaingia kazini kutokomeza ukeketaji

Muktasari:

Wazee hao kutoka koo za Inchugu, Inchage, Waryanchoka, Watatoga na Wangoreme wametoa ahadi hiyo baada ya kupatiwa elimu dhidi ya ukeketaji.

Serengeti. Vita dhidi ya ukeketaji imepata wenyewe, baada ya wazee wa kimila wa koo tano za kabila la Wakurya wilayani hapa, Mkoa wa Mara kuahidi kushiriki baada ya kubaini madhara yake.

Wazee hao kutoka koo za Inchugu, Inchage, Waryanchoka, Watatoga na Wangoreme wametoa ahadi hiyo baada ya kupatiwa elimu dhidi ya ukeketaji.

Mafunzo hayo yaliyoshirikisha makundi ya kijamii, yaliandaliwa na Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti kwa kushirikiana na Amref Health Africa Tanzania, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa ufadhili wa Kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia masuala ya wanawake (UN Women).

Mzee Joseph Mwita (73) kutoka Koo ya Waryanchoka amesema baada ya kushuhudia picha jinsi ukeketaji unavyotekelezwa, amegundua kuwa wanawake na watoto wa kike wanaofanyiwa vitendo hivyo hupitia maumivu na madhara makubwa kisaikolijia.

“Sisi wazee hatuhusiki moja kwa moja na tukio la ukeketeaji, bali jukumu letu ni kuweka sawa masuala ya kiufundi. Mangariba ndiyo hutekeleza jukumu la kukeketa na wamekuwa wakitueleza kuwa hawakati ila wanachanja tu,” amesema Mzee Mwita.

Kauli hiyo imeungwa mkono na Manjiwawi Ginaturu (79), kutoka ukoo wa Watatoga ambaye alisema baada ya mafunzo hayo, watashiriki kikamilifu vita dhidi ya ukeketaji.

Mzee kutoka ukoo wa Wangorime, Paulo Machumbe (90) amesema mafunzo waliyopewa na kushuhudia madhara ya ukeketaji wamegundua ni laana kuendelea kusimamia na kutetea mila hiyo.

Mwenyekiti wa wazee wa mila kutoka ukoo wa Inchugu Tanzania na Kenya, Masonoro Marwa (88) ameiomba elimu kuhusu madhara ya ukeketaji iendelee kutolewa kwa makundi ya jamii ya Wakurya na wanaojihusisha na ukeketaji ili kukomesha vitendo hivyo.

Mkuu wa wilaya hiyo, Nurdin Babu ameahidi kuwa Serikali itashirikiana na wazee hao kutekeleza azimio lao la kushiriki vita dhidi ya ukeketaji.