Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Korea kusaidia utekelezaji Dira 2050

Muktasari:

  • Miongoni mwa sekta zitakazoangaliwa  ni kilimo na uvuvi, utalii, ujenzi, madini, uchumi wa buluu, ubunifu, huduma za fedha na miundombinu ya barabara na chakula.
     

Dar es Salaam. Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Eunju Ahn amesema nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa maeneo makuu yaliyopewa kipaumbele kwenye Dira ya Maendeleo 2050.

Ametoa kauli hiyo leo Julai 4, 2025 wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Korea yaliyofanyika katika maonyesho ya 49 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DiTF).

Eunju amesema sekta hizo ni pamoja na kilimo na uvuvi, utalii, ujenzi, madini, uchumi wa buluu, ubunifu, huduma za fedha na miundombinu ya barabara na chakula.

“Tayari kampuni za Korea zinashiriki katika baadhi ya maeneo haya na zina nia ya kupanua zaidi uwekezaji,” amesema Eunju.

Alitumia nafasi hiyo kutangaza uzinduzi wa tawi la Tanzania la Chama cha Wafanyabiashara wa Korea Ughaibuni (OKTA), ambacho kinalenga kukuza biashara kati ya mataifa hayo mawili. OKTA ni mtandao wa kimataifa wa wafanyabiashara wa Korea wanaowekeza nje ya nchi.

“Hii ni hatua muhimu itakayosaidia kuvutia wawekezaji zaidi wa Korea nchini Tanzania,” amesema.

Alikipongeza chama hicho ambacho mwaka huu kinatimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake kwa kusaidia kukuza biashara kati ya nchi hizo mbili.

Katika kuonyesha utamaduni wa Korea, Baraza la Ushauri wa Muungano wa Amani (PUAC) liliandaa hafla ya kuonja vyakula vya asili vya Korea pamoja na maonesho ya kitamaduni, ikiwa ni njia ya kuimarisha uhusiano wa watu wa mataifa hayo mawili.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema Korea Kusini ni mfano wa kuigwa katika mafanikio ya haraka ya kiuchumi na Tanzania iko tayari kujifunza kutoka kwao hasa inapojipanga kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.

“Nilibahatika kuongozana  na Rais Samia Suluhu Hassan katika ziara yake nchini Korea Kusini mwaka jana. Moja ya maeneo yaliyonigusa sana ni Jumba la Makumbusho la Maendeleo lililopo Seoul. Korea ilikuwa nchi maskini, lakini leo ni miongoni mwa mataifa tajiri duniani”.

Amesema Tanzania inataka kuchukua somo kutoka mafanikio hayo ya Korea katika kutekeleza Dira ya Maendeleo 2050 ambayo tayari imepitishwa na Bunge na itazinduliwa rasmi Julai 17.

Profesa Mkumbo ametaja miradi kadhaa mikubwa ambayo Korea imeisaidia Tanzania, ikiwemo usambazaji wa mabehewa ya kisasa ya umeme kwa Reli ya Kisasa (SGR) na ujenzi wa Daraja la Urafiki la Tanzania na Korea maarufu kama Kigamboni Bridge.

Pia amesema nchi hizo mbili zimesaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wa jumla ya Dola za Marekani bilioni 2.5 (Sh6.62 trilioni) kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi (EDCF) ambao utasaidia kutekeleza miradi ya kipaumbele.

Kwa upande wake, Latifa Khamis, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), amesema kampuni zaidi ya 10 kutoka Korea zimeshiriki maonesho ya mwaka huu