Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kukauka mto Ruaha kwatishia uzalishaji umeme

Muktasari:

  • Hifadhi ya Ruaha na Selous ndio hifadhi kubwa zenye makundi ya wanyama wanaotembea kwa pamoja, hivyo kukosekana na kwa maji ni hatari wanyama hao wakafa au kuondoka kutokana na kukosekana kwa maji.

Mbarali. Mto Ruaha unaotajwa kuwa ni chanzo cha kuzalisha umeme katika vituo vya Kidatu, Kihansi na Mtera umekauka kiasi cha kushindwa kutiririsha maji, jambo linaloelezwa kuwa linatokana na shughuli za kibinadamu zinazofanywa kando ya mto zikiwemo za kilimo, na ufugaji.

 Wachambuzi na wadadisi wa masuala ya mazingira wanaeleza kuwa hali hiyo ikiendelea na kama mvua tacheleewa kunyesha, basi upo uwezekano wa kutokea kwa mgao wa umeme, kwani vituo hivyo vitatu vinavyotegemewa kwa ajili ya kufua umeme vitashindwa kuzalisha nishati hiyo.
Mwananchi Digital ikiwa na Kituo cha Wanahabari, Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA) imefika katika kijiji cha Ngiliama wilayani Mbarani Mkoa wa Mbeya (Bonde la Usangu) na kushuhudia mto huo ukiwa umekauka, huku kukiwa na ongezeko la shughuli za ufugaji na kilimo.
Akizungumza leo Novemba 4 katika hifadhi ya Ruaha, Mragibishi na Mdau Mazingira Msanii Selaman Msindi maarufu kwa jina la Afande Sele, amesema hifadhi hiyo inakabiliwa na ukame kutokana vyanzo vya maji kukauka katika mto huo ambapo kumesabishwa na mikono ya wanadamu.
Amesema kuwa ili kunusuru uoto wa asili katika  Mto Ruaha na Mbuga  inatakiwa jamii na watunga sera kuangaliwa kwa ukaribu na kupata utashi wa kisiasa katika kukabilina na athari hiyo.
Siku za karibuni Serikali ilitangaza uamuzi wa Baraza la Mawaziri kuhusu mgogoro wa eneo linalodaiwa kuwemo katika bonde la Ihefu wilayani Mbarali.
Uamuzi huo uliotangazwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Mabula ulipokewa kwa utulivu, lakini kwa hisia tofauti.
Katika uamuzi huo, Mabula aliyeambatana na Naibu Mawaziri watano wa sekta zenye maslahi na bonde hilo, alifuta vijiji vyote vitano vya Kata ya Luhanga na vitongoji 47 kutokana na uharibifu wa mazingira