Kuna uhusiano kati ya ukubwa wa injini ya gari, matumizi ya mafuta

Mafuta ni kimiminika muhimu kuliko vitu vyote katika gari. Ili gari liweze kufanya shughuli zake zilizoku­sudiwa ni lazima liwe na mafuta, ingawa siku hizo yapo yanayotumia gesi na umeme.

Uwepo wa mafuta hulifanya gari kutekeleza majukumu yake kama vile kuiwezesha mifumo mbalimbali ya gari kufanya kazi kwa ufasaha na kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Kwa kawaida kila gari hutumia kiwango fulani cha mafuta kwa kilo­mita moja, kulingana na ukubwa wa injini na umri wa gari lenyewe.

Ikiwa gari linatumia mafuta zaidi ya kiwango ilichotakiwa kutumia kwa umbali fulani, basi yawezekana kuna tatizo linalosababisha ongezeko hilo.

Kumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusu CC za gari na uhusiano wake katika ulaji wa mafuta wa gari. Kwe­nye Makala haya tutafahamu uhusia­no uliopo katika ya CC za gari lako, aina na utumiaji wa mafuta.

Gari kuwa na CC kubwa au ndogo hakuna uhusiano na aina ya mafuta inayotumia moja kwa moja bali aina ya mzigo ambao injini itakuwa ina­beba.

CC maana yake ni Cubic Centimeter yaani ni ukubwa au uwezo wa cylin­ders, ambamo mchanganyiko wa mafuta na hewa huchomwa.

Sasa kama gari lina CC kubwa lita­kuwa linatumia mafuta mengi kwa sababu ya ukubwa wa cylinder. Swali muhimu la kujiuliza ni CC inapati­kanaje?

Kwenye gari kuna kitu kinaitwa bore na stroke ambapo bore ni kip­enyo cha cylinder na stroke ni umbali ambao piston inatumia kusafiri juu hadi chini ya cylinder, yaani kwa kita­alamu inaitwa top dead center hadi bottom dead center.

Sasa ili kupata CC ya injini ya gari lako unachukua ujazo wa cylin­der moja unazidisha na idadi ya cylinder, kama gari lako lina piston 4 au 6 halafu unazidisha ila uhakikishe vipimo vyako vipo kwenye sentimita hapo utapata CC.

Kuhusu gari la petroli na dizeli ni kweli dizeli ni nafuu kwani hutumika kidogo kuliko petrol, ingawa mfumo wa kisasa wa injini za petroli ume­boreshwa kufanana na ule wa dizeli, yaani kutumia nozzel kuingiza mafuta kwenye cylinder, tofauti na carburetor hapo zamani.

Magari yenye injini za kisasa yote kama VVTI, D4-D, GDI n.k yana mfumo mzuri wa ulaji wa mafuta ambao ni wa kielektroniki na hata kama ni petroli inatumia nozzle na Petroli, mchangan­yiko wa hewa unafanyika kwa kubore­sha kiwango cha hewa zaidi kwenye chumba cha muwako, tofauti na zile za zamani ambapo ilikuwa mchanganyiko huo unafanyika ndani ya cylinder halafu unakuwa imewash­wa na plug.