Njia za kutambua muundo wa injini ya gari lako

Injini ni mashine muhimu kati­ka gari ambayo hubadili nishati kuwa mwendo unaotumiwa kwa kazi mbalimbali.

Umuhimu wa injini unatokana na kuliwezesha gari kuzalisha nguvu inayowezesha mifumo mbalimbali kufanya kazi.

Wakati wa kubadilisha nishati iliyomo kwenye mafu­ta ya petrol au dizeli, injini huzalisha joto kubwa kwa magari ya kisasa hadi nyuzi joto 4,000.

Kuifahamu injini ya gari lako kunaweza kukupa urahisi wa pale unapohitaji kununua vipuri vya injini.

Wapo watu wengi hawazifaha­mu injini za magari mao zipo katika muundo gani na hii hupelekea kuibiwa na mafundi wachache wasio waaminifu ila ukizifahamu walau kwa muundo itasaidia kukupa usalama zaidi.

Kuna njia kuu mbili za kufa­hamu injini ya gari ni ya namna/ muundo upi ambazo zinaweza kukupa urahisi katika utafutaji wa vipuri au injini yenyewe ambazo ni; visual inspection (kuitazama kwa macho) na manual books (kupitia kitabu cha gari).

Hizi ndiyo njia kuu mbili unazoweza kutumia kufahamu injini ni ya namna gani na hata nitakazoandika hapa zitakuwa zimetokea kwenye njia hizo mbili ila nakupa urahisi zaidi.

Ukiachana na hizo njia kuu mbi­li za kuifahamu injini hapa nitaku­wekea njia ndogo ndogo ambazo zinatokana na hizo njia kuu mbili.


Nishati inayotumia

Unaweza kuifahamu injini ya gari ni ya muundo gani kwa kuta­zama nishati inayotumia mfano (Diesel engine, Petrol engine na Natural gas engine) kupitia nisha­ti hizi unaweza kutambua injini ya gari ni ya namna gani.


Upoozaji

Unaweza kuifahamu injini ya gari kwa kupitia upoozaji wake unaofanywa kwe mfumo wa injini mfano (water/coolant cooling engine, air cooling engine) kupi­tia mifumo hii unaweza kuijua injini ya gari ni ya muundo upi, japo huku kwetu tume-shazoea mifumo ya water/coolant lakini ipo mifumo ya hewa pia.


Mifumo ya cylinder

Pia, unaweza kuijua injini ya gari kwa kuagalia mifumo ya cyl­inder ilivyowekwa kwenye injini mfano (inline vertical, horizontal, horizontal opposite, V type).


Ufanyaji kazi

Unaweza kuitambua injini kwa namna ya ufanyaji kazi wake kwani pia zinatofautiana kwenye utendaji kazi wake lakini hapa ni muhimu pia kumuona fundi kwa maelezo na elimu zaidi ila mfano wa utendaji kazi ni (rotary engine, piston engine na turbine engine).


Alphabet

Unaweza kuifahamu injini kupitia herufi zilizowekwa na waundaji wa injini ili kukupa urahisi zaidi mfano (2R, 3L, 2Y n.k). makala hii imejikita katika kuifahamu injini ya gari na si ufundi lakini kama unasumbuliwa na injini ya gari unaweza kutumia njia hizi kupata injini kwa urahisi au vipuri vyake.