Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

LHRC: Elimu ya Katiba miaka mitatu ni kupoteza muda

Mkurugenzi Mtendaji, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga 

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga amesema mpango wa kutoa elimu ya Katiba kwa miaka mitatu ni upotevu wa muda na rasilimali za Watanzania.

Henga ameyasema hayo leo Septemba 6, 2023 wakati akichangia kwenye mjadala wa Mwananchi X – Space ulioandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) ukiwa na mada inayosema: “Nini maoni yako kuhusu miaka mitatu ya elimu ya Katiba kwa wananchi?”

Ametoa hauli hiyo kufuatia msimamo wa Serikali liotolewa na aliyekuwa Waziri wa Katina na Sheria, Dk Damas Ndumbaro aliyesema kwamba Serikali inakusudia kutoa elimu ya katiba kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2023 – 2026.

Akichangia mjadala huo, Henga amesema mchakato wa Katiba ndiyo elimu yenyewe na yeye binafsi aliijua vizuri Katiba wakati mchakato ulipoanza kwa kuwa vyuoni hawafundishwi kwa kina, hivyo alijielimisha Katiba mbalimbali zilizopita nah ii ya sasa.

“Kuna watoto walikuwa wadogo hawakuwepo wakati Katiba inaandikwa lakini mbona hatukupewa elimu. Ndiyo maana kuna vitabu vya historia, kuna maktaba. Tuna resource (nyaraka) nyingi za kurejea,” amesema Henga.

Mkurugenzi huyo amesisitiza amejiuliza dhamira ya Serikali kutaka kutoa elimu hiyo nini lakini hajapata majibu. Amesisitiza kwamba Tume ya Jaji Joseph Warioba alikuwa akitoa elimu wakati akichukua maoni ya Watanzania, kwa hiyo inawezekana mambo hayo yakaenda sambamba.

Henga amebainisha Katiba nzuri inajengwa kwa maridhiano ya kitaifa na maridhiano hayo yafanyike kwa mchakato wa haki.

“Katiba nzuri ni katiba yenye maridhiano, hata mkichoka mnafanya mabadiliko ili mradi muwe mmeridhiana. Katiba siyo uzuri wa uandishi, ni hayo maridhiano, na maridhiano hayo yafuate mchakato wa haki,” amesema

Ameongeza Tume ya Thabiti Kombo iliyoandika Katiba ya CCM, ndiyo hiyo iliandika pia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1977, hivyo hakukuwa na uwakilishi wa wananchi katika zama ambazo chama kilikuwa kimeshika hatamu.