Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lissu: Ikipatikana Katiba mpya kigoma itapiga hatua kimaendeleo

Muktasari:

  • Lissu atoa somo kwa wananchi wa Wilaya ya Uvinza umuhimu wa kupata Katiba mpya itakayoondoa mfumo usiofaa wa kiutawala na kurejesha nguvu kwa watu huku akiwataka kuunga mkono harakati za upatikanaji wake.

Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amesema licha ya Mkoa wa kigoma kuwa sehemu muhimu katika uzalishaji mali kutokana na ardhi yenye rutuba lakini ni sehemu maskini iliyotelekezwa kwa kukosa maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na kiongozi huyo leo Jumapili Mei 21, 2023 akihutubia wananchi wa  Wilaya ya Uvinza mkoani hapo huku akieleza utelekezaji huo unatokana na nchi kutawaliwa na mfumo usiofaa unaopuuza maamuzi ya wananchi.

“Utaratibu wa Rais wa nchi yetu kuwa na madaraka makubwa kiasi cha kuamua kufanya anachotaka bila kubughuziwa na yeyote kutokana na Katiba tuliyonayo, limekuwa ni tatizo la kiutawala hadi viongozi wa mitaa wamekuwa miungu watu wakifanya ovyo hawachukuliwi hatua,”amesema.

 Amesema kutokana na hali hiyo viongozi wamekuwa wakifanya ufisadi mkubwa wa fedha za miradi ya maendeleo na hakuna hatua za makusudi zinazochukuliwa dhidi yao huku akitolea mfano mkoa wa Kigoma ni mkoa ambao unashikilia rekodi ya kutofunguliwa kimiundombinu ya barabara ya lami kwenda mikoa mingine.

“Jambo kama hili linashangaza haiwezekani tangu nchi ipate uhuru ukizunguka mikoa yote Kigoma iko nyuma kimaendeleo lakini una ardhi safi huku wananchi wake wakitaka kusafiri njia pekee ni kutumia reli iliyojengwa na mkoloni,”ameongeza.

“Kigoma ni mkoa maskini kuliko mikoa yote nchini mnafikiri nini na mmemkosea nini Mungu wakati mnatafakari hilo tambueni Kigoma unashika rekodi ya kutokuunganishwa kwa barabara za lami na mikoa mingine,”amesema

Lisu amesema hakuna njia nyingine ya kumaliza tatizo hilo zaidi ya kuhakikisha Wananchi wengi wanaungana na kupata Katiba mpya itakayoondoa tabia hiyo kwani Taifa haliwezi kupiga hatua kimaendeleo kama mfumo uliopo hautaondolewa.

“Wananchi wote wanaopitia maumivu ya maisha ni wakati wa kuunga mkono harakati za kudai katiba mpya ili kupata suluhu ya matatizo yaliyopo kwa kugawanya madaraka,” amesema.