LIVE: Uzinduzi kitabu cha maisha ya Mkapa wawakutanisha vigogo Dar

LIVE: Uzinduzi wa Kitabu cha Rais mstaafu Benjamin Mkapa (My life my purpose)

Muktasari:

Uzinduzi wa kitabu cha maisha binafsi ya Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa umewakutanisha viongozi wastaafu na waliopo madarakani..

Dar es Salaam. Uzinduzi wa kitabu cha maisha binafsi ya Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa umewakutanisha viongozi wastaafu na waliopo madarakani.

Uzinduzi huo unafanyika leo Jumanne Novemba 12, 2019 katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli ndio mgeni rasmi katika uzinduzi huo.

Viongozi wa dini, waandishi wa habari, mabalozi, viongozi wastaafu, waliopo madarakani ni kati ya waliohudhuria uzinduzi  wa kitabu hicho cha Maisha Yangu, Kusudio Langu.

Baadhi ya waliohudhuria ni marais wastaafu wa Tanzania, Ally Hassan Mwinyi na Jakaya Kikwete na Rais wa  Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.

Wengine ni waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa;  Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma; Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai;  katibu mkuu kiongozi wa Tanzania, Balozi John Kijazi na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Pia wapo  makamu wa kwanza wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad; Jaji mkuu mstaafu, Othman Chande na mama Ana Mkapa, mke wa rais huyo wa Awamu ya Tatu.

Mkapa amezaliwa Novemba 12, 1938 Ndanda wilayani Masasi mkoani Mtwara.

Uzinduzi huo unafanyika leo siku ambayo kiongozi huyo mstaafu anasherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 81.