Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lukuvi, Kabudi warejeshwa Baraza la Mawaziri, Ummy, Kairuki wang’olewa

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali, wakiwemo William Lukuvi na Profesa Palamagamba Kabudi ambao wamrejeshwa kwenye Baraza la Mawaziri.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Moses Kusiluka, pamoja na wawili hao viongozi walioteuliwa na kuhamishwa vituo vya kazi ni kama ifuatavyo:


Uteuzi wa mawaziri

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Sharifa Nyanga, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu imesema Profesa Kabudi ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, huku Lukuvi akiteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Taarifa hiyo iliyotolewa leo Agosti 14, 2024 imesema Jenista Mhagama ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya kuchukua nafasi ya Ummy Mwalimu, kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Pia amemteua Balozi Pindi Chana kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, awali alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Anachukua nafasi ya Angellah Kairuki, aliyeteuliwa kuwa Mshauri wa Rais.


Mwanasheria Mkuu

Rais Samia pia ameteua Hamza Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuchukua nafasi ya Jaji Eliezer Feleshi, ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.  Kabla ya uteuzi huo Johari alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Samwel Maneno, ameteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, awali alikuwa Msaidizi wa Rais, Sheria. Anachukua nafasi ya Balozi Kennedy Gastorn ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais, Sheria na Mikataba.

Mteule mwingine ni Dk Ally Possi ambaye anakuwa Wakili Mkuu wa Serikali, kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi.

Mbali ya hao, Rais Samia pia ameteua  Salum Hamduni kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Hamduni anachukua nafasi ya Profesa Siza Tumbo ambaye amerejea Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).

Rais pia amemteua Ismail Rumatila kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, awali alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Mwingine aliyeteuliwa na Rais ni Atupele Mwambene anayekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia masuala ya elimu. Kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Rais Samia amemteua Abdul Mhinte kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia mifugo. Kabla ya uteuzi alikuwa Ofisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu.

Pia Methusela Ntonda ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, kabla ya uteuzi huo alikuwa Ofisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu.


Uhamisho wa naibu makatibu wakuu

Dk Grace Magembe amehamishwa kutoka Wizara ya Afya kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia masuala ya afya.

Dk Charles Msonde amehamishwa kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, huku Dk Wilson Charles amehamishwa kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, anayeshughulikia masuala ya elimu ya msingi na sekondari.

Profesa Daniel Mushi amehamishwa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia masuala ya sayansi na elimu ya juu.

Dk Franklin Rwezimula amehamishwa kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, huku Dk Khatibu Kazungu amehamishwa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya umeme na nishati jadidifu.

Katika uteuzi huo, Dk James Mataragio aliyewahi kuwa mkurugenzi kuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli  (TPDC), anakwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya petroli na gesi, huku Ludovick Nduhiye akihamishwa kutoka Wizara ya Ujenzi kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi.

Dk Suleiman Serera amehamishwa kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo anayeshughulikia masuala ya ushirika na umwagiliaji.

Taarifa imesema Dk Hussein Mohamed Omar atakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo anayeshughulikia masuala ya maendeleo ya mazao na usalama wa chakula.


Wakuu wa wilaya wahamishwa

Rais amemhamisha Kanali Maulid Surumbu kutoka Wilaya ya Tarime kwenda Mbarali, akichukua nafasi ya Brigedia Jenerali Denis Mwila ambaye amepangiwa majukumu mengine.

Meja Edward Gowele amehamishwa kutoka Rufiji kwenda Tarime, huku James Kaji akihamishwa kutoka Tanga kwenda kuwa Moshi.

Zephania Sumaye amehamishwa kutoka Wilaya ya Moshi kwenda Lushoto, huku Japhari Mghamba amehamishwa kutoka Wilaya ya Lushoto kwenda Wilaya ya Tanga.

Rebecca Msemwa amehamishwa kutoka Wilaya ya Morogoro kwenda Bahi, huku Gift Msuya kutoka Bahi kwenda Pangani na Mussa Kilakala kutoka Wilaya Pangani kwenda Wilaya ya Morogoro.

Rais samia pia amefanya uteuzi wa katibu tawala wa wilaya, ambao Proscovia Mwambi ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukoba.


Uhamisho wa ma-DED

Rais amefanya uhamisho wa wakurugenzi watendaji wa halmashauri wafuatao:

John Kayombo amehamishwa kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Juma Seph amehamishwa kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha kwenda Jiji la Tanga, huku Fredrick Sagamiko akihamishwa kutoka Jiji la Tanga kwenda Dodoma.

Elihuruma Mabelya amehamishwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Jomary Satura amehamishwa kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwenda Manispaa ya Temeke, huku Joanfaith Kataraia amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kwenda Manispaa ya Singida.

Jeshi Godfrey Lupembe amehamishwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Singida kwenda Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, huku Khamis Katimba akihamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi.

Rose Manumba amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kwenda Wilaya ya Msalala huku Stephen Katemba akihamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwenda Mbarali.

Missana Kwangura amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kwenda Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga; huku Happines Msanga akihamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwenda Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe; na Dk Amon Mkoga amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.


Wakuu wa taasisi nao wamo

Rais Samia amepangua pia wakuu wa taasisi alimteua Crispin Chalamila kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Kabla ya uteuzi alikuwa Ofisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu.

Moremi Marwa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), kabla ya uteuzi alikuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Magereza (Shima); na Dk Irene Isaka ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) akichukua nafasi ya Bernard Konga anayedaiwa mkataba wake umemalizika.

Taarifa imesema uapisho wa mawaziri, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Katibu Tawala wa Mkoa na Naibu Makatibu Wakuu wateule utafanyika Ikulu ya Dar es Salaam kesho Agosti 15, 2024 saa nane  mchana.


Kama una maoni kuhusu habari hii, tuandikie ujumbe kupitia WhatsApp: 0765864917.