Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madiwani Bukombe wahofia kupoteza miradi ya maji

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wakipitia taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji vijiji inayo tekelezwa na RUWASA abapo wamebaini taarifa hiyo inamapungufu na kuhofia badhi ya miradi ya maji kipotea. Picha na Ernest Magashi.

Muktasari:

  • Madiwani wa Bukombe wamehoji sababu za kusuasua kwa miradi ya maji, hata hivyo, kaimu meneja wa Ruwasa wilaya ya Bukombe, James Benny amekiri jambo hilo na kueleza kwamba limesababishwa na mabadiliko ya kutangaza zabuni.

Bukombe. Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe mkoani Geita wameonyesha hofu ya kupoteza baadhi ya miradi ya maji katika halmashari hiyo kutokana na kucheleweshwa kwake.

Hoja hiyo imeibuliwa leo Februari 18, 2022 kwenye baraza la madiwani na baadhi ya madiwani baada ya kupokea taarifa ya miradi ya maji inayotekelezwa na Ruwasa.

Diwani wa kata ya Ushirombo, Lameck Warangi amesema miradi inasuasua kujengwa katika halmashauri hiyo, mfano mradi wa maji wa Mwalo tangu Mei 2021 hadi leo hakuna kinachoendelea na fedha zinaenda kuingia bajeti nyingine, hali ambayo inaweza kusababisha mradi huo kupotea.

Amesema wananchi wanahofia kupoteza mradi huo ambao utawatoa katika hali ya sasa ya kunywa maji pamoja na ng'ombe wakati serikali imetoa fedha.

Hoja hiyo iliungwa mkono na diwani wa kata ya Lyambamgongo, Boniphace Shitobelo ambaye alisema kwenye kata yake kuna mradi una muda mrefu lakini ujenzi unasuasua na mkandarasi alionekana saiti miezi sita iliyopita.

Kaimu meneja wa Ruwasa wilaya ya Bukombe, James Benny alisema ni kweli miradi inasuasua lakini ni kutokana na mabadiliko ya kutangaza zabuni. Amesema zamani walikuwa wanabandika kwenye mbao za matangazo lakini utaratibu ukabadirika kutaka matangazo yanatolewa kwenye mifumo na wakandarasi wakawa na changamoto ya kuingia kwenye mifumo hiyo.

Benny amesema kwa mwaka wa fedha 2021/2022, wilaya ya Bukombe ilipanga kutumia Sh3.7 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji ikiwa miradi mipya na miradi viporo.

Benny amesema hadi sasa fedha iliyopokelewa ni Sh2.1 bilioni sawa na asilimia 56 ya bajeti huku fedha iliyovuka mwaka (bakaa) ni Sh245.7 milioni na kufanya fedha iliyopokelewa na bakaa kuwa ni Sh2.3 bilioni.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Bukombe, Yusuph Mohamed amesema miradi ya maji wilaya ya Bukombe inajengwa kwa kusuasua na madiwani walitarajia kupata taarifa ya maji mjini na vijijini lakini imekuja taarifa ya vijijini huku mjini Ushirombo kuna miradi mikubwa ukiwemo wa Sh700 milioni hawajui hatima yake.

Mohamed alimuomba kaimu meneja wa Ruwasa kubadilika na kuhakikisha miradi inakamilika na fedha zisivuke mwaka wa fedha kwenda mwaka mwingine.