Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahakama yawaachia huru Gugai na wenzake

Mahakama imewaachia huru Gugai na wenzake

Muktasari:

  •  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa mhasibu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai na wenzake wawili baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.


Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa mhasibu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai na wenzake wawili baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Gugai na wenzake walikuwa wanakabiliwa na makosa 40, makosa 19 kati ya hayo ni kughushi, 20 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali.

Gugai alikuwa anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Januari 2005 na Desemba 2015.